20/10/2023
SANAMU YA MWL. JK NYERERE.
Sanamu hii iliyotengenezwa kwa madini ya chuma inayoonesha twasira ya Mwl. JK Nyerere alipewa na Wajerumani k**a zawadi mwaka 1966, baada ya kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania.
Na hapa ilipo ni sehemu ambapo Mwl. Nyerere alipozaliwa, na hapa ndipo nyumba ya Bi Christina Mgaya Nyang'ombe Mama yake na Mwl. JK Nyerere ilipokuwa, ilikuwa imejengwa kwa tope juu yake ikiwa imeezekwa kwa Nyasi.
Zamani Zahanati na hospitali hazikuwa nyingi k**a ilivyo kwa sasa ambapo kila sehemu zimeenea, hivyo Wamama walikuwa wanajifungulia tu ndani k**a kawaida baada ya hapo kitovu au kondo la mtoto huzikwa ndani ya Nyumba.
Na sanamu hii imewekwa hapo kwaajili ya kuenzi uzao wa Bi Christina Mgaya Nyang'ombe na Mwl. JK Nyerere ambapo ndipo kitovu Mwl. Nyerere au kondo lake lilipozikwa au kufukiwa.
Tembea kwenye makazi ya Mwl. JK Nyerere (MWITONGO).
Culture is Beautiful 💖💖💖, Culture is Incredible 💫💫💫
🇹🇿 .tanzania
Follow me
https://instagram.com/mpina_jeremiah?utm_source=qr&igshid=MThlNWY1MzQwNA==