Daniel Mlamka

  • Home
  • Daniel Mlamka

Daniel Mlamka Professional Tour Guide in Nature & Cultural Experience | Adventures | Farm Tours
Tell: +255674217445
(1)

Kila Binadamu na Mzigo Wake, Lakini huu wangu nahisi kuna Mtu kaniongezea🥺😤
24/05/2024

Kila Binadamu na Mzigo Wake, Lakini huu wangu nahisi kuna Mtu kaniongezea🥺😤

03/05/2024

Je, unatamani Weekend au Siku za Wiki Ufike hapa...?
Bofya Kitufe kilichoandikwa WhatsApp upande wa Kulia chini ya Video hii au Tembealea Gwankaja Farm Lodge kwa Maelezo Zaidi

Matema (Mwalalo) Waterfall 💦📍 Kyela District, in Mbeya Tanzania 🇹🇿Maporomoko ya Maji Matema/Mwalalo 💦 yenye Maji Masafi ...
19/04/2024

Matema (Mwalalo) Waterfall 💦

📍 Kyela District, in Mbeya Tanzania 🇹🇿

Maporomoko ya Maji Matema/Mwalalo 💦 yenye Maji Masafi ni Maporomoko yanayopatikana Kwenye Mto Mwalalo unaotokea kwenye Safu za Milima Livingstone na kumwaga Maji yake Ziwa Nyasa kupitia Matema Beach, iliyopo Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya Tanzania 🇹🇿

Ingawa kuna baadhi ya Sehemu panakupa changamoto Chanya (Adventures), ila Kuyafikia Maporomoko haya kunakupa Uzoefu wa wa kipekee na wa Kufurahisha kwani sio wa Kuchosha, sababu unapita Mwambaoni mwa Mto huo na kukutana na hali ya Ubaridi Murua kabisa hadi utakapoyafikia Maporomoko haya💦

Ukifika kwenye Maporomoko haya unaweza kufanya shughuli mbalimbali za kukutunzia Kumbukumbu isiyosahaurika k**a Kuogelea, kupiga picha na mengine mengi kadili utakavyopendelea👐

K**a Unatamani Kujua Maelezo Zaidi au Kufika hapo Bofya Palipoandikwa WhatsApp chini ya picha hii Kulia👇👇

Isabula Waterfall 💦📍 Rungwe District, in Mbeya Tanzania 🇹🇿Maporomoko ya Maji Isabula 💦 Maporomoko ya Amani👐  Unaweza Pat...
18/04/2024

Isabula Waterfall 💦

📍 Rungwe District, in Mbeya Tanzania 🇹🇿

Maporomoko ya Maji Isabula 💦 Maporomoko ya Amani👐 Unaweza Pata Uzoefu ukiwa Juu yanaokoanzia kuanguka na Chini yanakoangukia😍

K**a Unatamani Kujua Zaidi au Kupelekwa hapo Bofya Palipoandikwa WhatsApp chini ya picha hii Kulia👇👇

19/03/2024

Hii nini sasa...???😨🤣🤣🤣🤣🤣🤗

📍Isabula Waterfall | Maanguko ya Isabula:Maanguko haya yanapatikana Kitongoji cha Iseselo, Kijiji cha Isabula, Wilaya ya...
11/03/2024

📍Isabula Waterfall | Maanguko ya Isabula
:
Maanguko haya yanapatikana Kitongoji cha Iseselo, Kijiji cha Isabula, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya Tanzania katika Mto Mwalisi unaoungana na Mto Mbaka na mito mingine Kumwaga Maji yake Ziwa Nyasa🌊

Inafikika kirahisi mno kwa Gari/Pikipiki/Kutembea hadi sehemu maporomoko yalipo
Inakuchukua Takribani 5 Km kutokea barabara kuu ya Tukuyu- Busokelo (Lwangwa/Lufilyo/Ntaba) au Ipinda/Matema Beach 🏖️

Ukisikiliza simulizi mbalimbali toka kwa wenyeji wa Kijiji cha Isabula hasa Wazee, wanasimulia Kuna mtu alikua ana tabia ya kutoa/kuharibu Mimba kila anapopata Ujauzito (Mimba), baada ya kush*tukiwa na watu hasa waliofanyiwa hivo, kuwa anafanya unyama huo, aliamua kujitupa katika Maporomoko haya, ili afe kukwepe kesi hiyo inayomkabili, basi maporomoko haya kwa kuwa yanapenda Amani🤗, yalimshusha na kumvutia pembezoni akiwa mzima kabisa, hivo mama hakuweza kutimiza haja yake ya kujiua, akawa mzima😜

Kitu cha kufurahisha zaidi, unaambiwa kwamba k**a umeenda kwa nia mbaya k**a kuua au kujiua kupitia maporomoko haya, basi unajidanganya ahahaha, kwa maana hutaweza fanikisha azimio lako hilo ovu😝

What a waterfall?😍

📸 Mponjoli (mpoafrka)🙏
:
Follow Daniel Mlamka Daniel Mlamka kwa Tips za Kutalii


📍Itende Crater Lake, in Busokelo Rungwe Mbeya Tanzania 🇹🇿Moja ya Maziwa ya Kreta Mkoa wa Mbeya, lililopo Wilaya ya Rungw...
09/03/2024

📍Itende Crater Lake, in Busokelo Rungwe Mbeya Tanzania 🇹🇿

Moja ya Maziwa ya Kreta Mkoa wa Mbeya, lililopo Wilaya ya Rungwe Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye Muonekano wa kufanana na Ziwa Ngosi kwa mbali

Ziwa hili lipo kwenye Safu za mlima Ngululwale, na Ukiwa Ziwani hapo unaweza kuona Muonekano mzuri Ziwa la Kreta Kisiba/Masoko Upande wa Magharibi, Ikapu/Mbambo, Kingili na Ziwa Nyasa Upande wa Kusini Mashariki na maeneo kadha wa kadha

Unaweza kufika Ziwani hapa kwa njia kuu Tatu
1. Kutoka Mbambo (Mto Mambwe), Kupanda mlima kwa Takribani Masaa 2⛰️🚶.....Njia nzuri kwa wanaopendela changamoto kwenye hiking

2. Kuingilia Mzalendo au Njiapanda ya Itete ambapo toka utakapoacha Usafiri wako unatembea Dk 45 Takribani Kilomita 1.5 kulifikia Ziwa hili ⛰️🚶.....Njia Nzuri haina Changamoto nyingi na unaweza amua kupita kwenye Daraja la Mungu (Kivutio Kingine)🤗

3. Kutokea Kijiji cha Ngululwale kushuka chini hadi Ziwani.......Njia Rahisi maana ni Kushuka tu 🚶⛰️

K**a unahitaji Kutembelea Ziwa hili na Vivutio vilivyondani ya Busokelo Fika Gwankaja Farm Lodge ✌️



📍Itende Crater Lake, in Busokelo Rungwe Mbeya Tanzania 🇹🇿Moja ya Maziwa ya Kreta Mkoa wa Mbeya, lililopo Wilaya ya Rungw...
08/03/2024

📍Itende Crater Lake, in Busokelo Rungwe Mbeya Tanzania 🇹🇿

Moja ya Maziwa ya Kreta Mkoa wa Mbeya, lililopo Wilaya ya Rungwe Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye Muonekano wa kufanana na Ziwa Ngosi kwa mbali

Ziwa hili lipo kwenye Safu za mlima Ngululwale, na Ukiwa Ziwani hapo unaweza kuona Muonekano mzuri Ziwa la Kreta Kisiba/Masoko Upande wa Magharibi, Ikapu/Mbambo, Kingili na Ziwa Nyasa Upande wa Kusini Mashariki na maeneo kadha wa kadha

Unaweza kufika Ziwani hapa kwa njia kuu Tatu
1. Kutoka Mbambo (Mto Mambwe), Kupanda mlima kwa Takribani Masaa 2⛰️🚶.....Njia nzuri kwa wanaopendela changamoto kwenye hiking

2. Kuingilia Mzalendo au Njiapanda ya Itete ambapo toka utakapoacha Usafiri wako unatembea Dk 45 Takribani Kilomita 1.5 kulifikia Ziwa hili ⛰️🚶.....Njia Nzuri haina Changamoto nyingi na unaweza amua kupita kwenye Daraja la Mungu (Kivutio Kingine)🤗

3. Kutokea Kijiji cha Ngululwale kushuka chini hadi Ziwani.......Njia Rahisi maana ni Kushuka tu 🚶⛰️

K**a unahitaji Kutembelea Ziwa hili na Vivutio vilivyondani ya Busokelo Fika Gwankaja Farm Lodge ✌️



23/02/2024

Mungu alituumbia Vitu mbalimbali vya kututoa Stress na kutufanya tukumbuke na Kushuhudia Ukuu, Upendo na Uweza wake

📸 Nicolas Schn

📍 Mwalalo Waterfall 💦 Matema Kyela Mbeya Tanzania

On the way to Itende Crater Lake📍Busokelo, Rungwe District Mbeya Tanzania 📸 Nicolas Schn 🙏
23/02/2024

On the way to Itende Crater Lake

📍Busokelo, Rungwe District Mbeya Tanzania

📸 Nicolas Schn 🙏

Tuliambiwa Huu Mwaka Tutaitwa maBosi😅....... February hii inaishia hata Sijaitwa Bosi hata ya Utani😭Huu Mwaka 2024 Ushan...
18/02/2024

Tuliambiwa Huu Mwaka Tutaitwa maBosi😅....... February hii inaishia hata Sijaitwa Bosi hata ya Utani😭

Huu Mwaka 2024 Ushanishinda, Na-zoom 2025 nione ipoje👐

Kuna mda unajiuliza Mbona Mungu anawaondoa Marafiki zako, wanaokuzunguka na mlikua mnaivana vizuri tu, lakini mara gafla...
30/12/2023

Kuna mda unajiuliza Mbona Mungu anawaondoa Marafiki zako, wanaokuzunguka na mlikua mnaivana vizuri tu, lakini mara gafla hawakutafuti, hawakujali inshort wamekupotezea🤔

Mungu amewaondoa hao Sababu ame/anasikia na anajua Mipango/Maongezi yao Mabaya wanayojadilli kuhusu wewe. Order👐

Tuwaache Waende Zao👐


Kuna Mda Binadamu wanafikilia kwamba hatuwezi kuishi bila Misaada/Sapoti YAO.... Tuwakumbushe Kuwa Kabla YAO Tulikuwa  H...
21/12/2023

Kuna Mda Binadamu wanafikilia kwamba hatuwezi kuishi bila Misaada/Sapoti YAO.... Tuwakumbushe Kuwa Kabla YAO Tulikuwa Hatuwajui na Tuliishi Vizuri tu.....

Sometimes we need to get out of our Usual Home place and go explore new somewhere 😊
30/11/2023

Sometimes we need to get out of our Usual Home place and go explore new somewhere 😊

Hao ndio Walimwengu, Ukifa, Siku ya Msiba wako wanachangia Mapesa Mengi tu tena  Kwahiari, Ni kweli na Ajabu Wakati Unau...
19/08/2023

Hao ndio Walimwengu, Ukifa, Siku ya Msiba wako wanachangia Mapesa Mengi tu tena Kwahiari,
Ni kweli na Ajabu Wakati Unaumwa hawakukuchangia (au walikuletea tu machungwa)😱😭

Tungechangia ili Apone ingekua Heri zaidi ya Kuchangia Akifa🤝

Tutafute huku Tunaishi (tulivyonavyo viwafaidishe na wenzetu wasioanavyo) kwa maana Hatutaenda na Chochote🤝👐
14/08/2023

Tutafute huku Tunaishi (tulivyonavyo viwafaidishe na wenzetu wasioanavyo) kwa maana Hatutaenda na Chochote🤝👐



  , Tutafute & Tujenge Pamoja
10/08/2023

, Tutafute & Tujenge Pamoja

Heri ya Sikukuu ya Wakulima Tanzania | NanenaneFor more tourism tips Follow     Daniel Mlamka
08/08/2023

Heri ya Sikukuu ya Wakulima Tanzania | Nanenane

For more tourism tips Follow Daniel Mlamka

Ukikutana na   Fanya Hivi👇👇Usisogee Karibu yake Pia Usimbugudhi:Tembo Ukimsogelea jirani na kuanza kumbugudhi kwa kuones...
02/08/2023

Ukikutana na Fanya Hivi👇👇

Usisogee Karibu yake Pia Usimbugudhi:
Tembo Ukimsogelea jirani na kuanza kumbugudhi kwa kuonesha ishara yeyote ya kutaka kumdhuru, huhisi anavamiwa hivo hukasirika na kuanza kukufukuza

K**a anakufukuza toa nguo zako k**a shati ama koti kisha mrushie, atatumia muda mwingi kushughulika na nguo hizo huku ukitafta uelekeo wa kumkwepa

Panda kwenye Mti Mkubwa:
Tembo ni Mnyama mwenye nguvu na akili, hivo anaweza vunja miti midogo hata mikubwa kiasi, Hivo Unapaswa ukiweza Panda kwenye mti mkubwa ambao hauwezi angushwa na Tembo

Kimbilia Uelekeo wa Upepo:
Tembo hutambua uwepo wako hata k**a huonekani kwa kunusa Harufu ya Adui yake (wewe), Hivo Unapaswa kutambua uelekeo wa upepo na kuhakikisha Unakimbia kuelekea unakoelekea Upepo sio unakotok upepo (Kwa maana kwamba hakikisha upepo kutoka kwako hauelekei alipo tembo)

Follow for More Wild Tips





Miaka 125 imetimia jana tarehe 19 July 2023:Siku ya jana  Tarehe 19 July 2023 imetimia Miaka 125 ya Chief Mkwavinyika Mu...
21/07/2023

Miaka 125 imetimia jana tarehe 19 July 2023
:
Siku ya jana Tarehe 19 July 2023 imetimia Miaka 125 ya Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga
maarufu k**a "Chief Mkwawa" tangu siku ya kifo chake (19 July 1898)

Mkwawa aliku ndie chief wa kwanza kwa uMaarufu wa Wahehe kutoka Iringa, na Umaarufu wake unatokana na Akili na Ushupavu wake katika uongozi wake na kupelekea kushinda vita yake dhidi ya wavamizi wa Kijerumani

18/07/2023

Magnificent falls that you can enjoy while at the top and bottom of the falls

In Rungwe district, Mbeya Tanzania

Tanzania National Parks (TANAPA) Tanzania Wildlife Management Authority - TAWA Tanzania Unforgettable Tanzania Forest Services Agency Rungwe Yetu

Mazingira Kwetu Sio Kikwazo💪Kati ya michezo inayopendwa na watu wengi hasa Vijana ni pamoja na mchezo wa Pool TableWatot...
06/06/2023

Mazingira Kwetu Sio Kikwazo💪

Kati ya michezo inayopendwa na watu wengi hasa Vijana ni pamoja na mchezo wa Pool Table

Watoto hawa (Darasa la Kwanza hadi Kidato cha 4) hawajabaki nyuma katika mchezo huu, nao wameona Mazingira kwao yasiwe Kikwazo cha kuwanyima Furaha yao pendwa😋 kwa kuamua Kujiongeza Kiubunifu na kuunda Pool Table yao ya Kinu, Mbao, Kitambaa, Misumari pamoja na Mipira/Minati k**a Quisieni/Kwisheni/kusheni🤗👍🔥

Location: Kijiji cha Ubiri, huko Turiani wilaya Mvomero Morogoro Tanzania

 : Sisi tunawakumbuka kwa kuwapigia simu au kwa SMS kwasababu tunajali THAMANI ya UWEPO WAO🤼🎊.. Ila wao wanatukumbuka wa...
14/03/2023

: Sisi tunawakumbuka kwa kuwapigia simu au kwa SMS kwasababu tunajali THAMANI ya UWEPO WAO🤼🎊..
Ila wao wanatukumbuka wakiwa na SHIDA ZAO😭

Hamnipati ng'oooo 🤪✋ (Ukiwa na shida nitafute wiki 2 kabla hujasema shida yako hapo sawa)🫣😜

14/02/2023

Tunashukuru siku ya Valentine imeisha vizuri maana AMETUPA FARAJA.... isingekua hivo tungezungumza mengine

Isabula Waterfall | Maporomoko ya Maji Isabula Rungwe Mbeya🌊😋Unatamani kufika na hujui unafikaje wasiliana nasi kwa kubo...
13/02/2023

Isabula Waterfall | Maporomoko ya Maji Isabula Rungwe Mbeya🌊😋

Unatamani kufika na hujui unafikaje wasiliana nasi kwa kubofya Batani iliyoandikwa WhatsApp kulia chini ya picha hii👇👇

For more information click the WhatsApp button bellow this photo👇

Or Follow our social media pages Daniel Mlamka (Facebook & Instagram)

  Tanzania na Afrika MasharikiEneo hili lipo Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, likipakana na Bahari ya HindiKatika Historia ya Uk...
07/02/2023

Tanzania na Afrika Mashariki

Eneo hili lipo Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, likipakana na Bahari ya Hindi
Katika Historia ya Ukristo Tanzania ulioenezwa na wamisionari miaka mingi iliyopita (k**a wengi tulivosoma darasani katika somo la Historia) basi Wamisionari hao waliingia Tanzania/Afrika Mashariki kupitia sehemu hii ulipojengwa , ndio maana panaitwa LANGO LA UKRISTO, pia wakajenga la Kwanza (la Kikatoliki) Tanzania (pichani) ndipo taratibu wakaanza kieneza Ukristo nchi nzima na Afrika Mashariki

Ikumbukwe kwa Mji wa Bagamoyo pia lilikua pia lango la Biashara ya Utumwa na Palikua na Soko la watumwa, ambapo hadi leo jengo hilo la Soko na jengo ambalo lilitumiwa kuwapumzisha watumwa kabla ya kuuzwa (Caravan Serai) lipo kwa ajili ya makumbusho)

Kwa namna moja ama nyingine Wamisionari hao walikua wanapinga vikali Biashara ya Utumwa iliyokua imeshamili Tanzania na Afrika nzima
Hivo basi baadhi ya watumwa waliokua wakichukuliwa kwenye mikoa ya kusini, katikati na sehemu zingine Tanzania k**a kigoma Tabora nk, walinunuliwa sokoni hapo na wamisionari na kutunzwa kituoni lilipo Kanisani hilo

Wakristo Wakatoliki wanatumia sehemu hii k**a kituo chao cha , ambapo hutembelea kituo hiki baada ya mda fulani kwa ajili ya Ibada na kujifunza mambo kadha wa kadha yahusuyo Wamisionari, Ukristo, Imani, Utumwa na Elimu Dunia

Lakini pia watu wengine (Watembezi/wasafiri/Watalii) hutembelea eneo hili kujifunza au kujikumbusha, kwani pamewekwa Jengo maalumu la Makumbusho lililosheni historia yote ya Wamisionari na Ukristo Tanzania na Afrika Mashariki

K**a Bado, nakushauri utembelea Eneo hili...utanishukuru baadae

amewahi tembelea eneo hili...?
Je, Ulitembelea k**a Mtalii, au ulienda Hija..?

Mpiga picha 📸: 🙏

Follow FB: Daniel Mlamka IG: Daniel_explore

Uyoga | Mushrooms 🍄😋
15/12/2022

Uyoga | Mushrooms 🍄😋

 🇹🇿UHURU NA KUUTUMIKIA UHURU
09/12/2022

🇹🇿

UHURU NA KUUTUMIKIA UHURU

Hakuna RAFIKI anayebadirika kuwa ADUI, huyo alikua Adui toka mwanzo Sema ulichelewa tu kujua🧐K**a ni rafiki atakua rafik...
19/11/2022

Hakuna RAFIKI anayebadirika kuwa ADUI, huyo alikua Adui toka mwanzo Sema ulichelewa tu kujua🧐

K**a ni rafiki atakua rafiki tu milele, HAIJALISHI

Picha haihusiani na Ujumbe👐😂

😂

Direct Drinking Water from Kaporogwe Waterfall 😋💧💦 in Rungwe Mbeya TanzaniaThat Experience 😊💥Interested to visit here, y...
09/11/2022

Direct Drinking Water from Kaporogwe Waterfall 😋💧💦 in Rungwe Mbeya Tanzania

That Experience 😊💥

Interested to visit here, you're welcome 🙏

Address

Gwankaja Farm Lodge

Telephone

+255674217445

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Daniel Mlamka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Daniel Mlamka:

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Travel Agency?

Share