
06/12/2023
Chikanda safaris kwa kushirikiana na Hifadhi ya Mpanga kipengere leo siku ya jumatano ya tarehe 06/12/2023 tumezindua kampeni ijulikanayo k**a Mpanga kipengere uni retreat katika chuo cha utumishi wa Umma.
Uzinduzi huu uliudhuliwa na Mkuu wa Hifadhi ya Mpanga kipengere Donasian Makoi, Afisa Utalii Adelard Tesha, Serikali ya wanafunzi chuo cha utumishi wa Umma, Mkurugenzi Chikanda safaris Amos Mwamugobole, Mkurugenzi Mazplusfly Zakaria Mgallah, pamoja na Mkurugenzi wa Photobank studio Exavery Mwakagali
Lengo la kampeni hii ni kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vya Mkoa wa Mbeya kuweza kutembelea Hifadhi ya Mpanga Kipengere iliyopo kati ya mkoa wa Mbeya na Njombe.