11/11/2024
*Wazee wanasema "K**a umebeba chungu cha asali, usimuonee wivu aliyebeba pingili mbili za miwa". Kuna watu kwenye maisha Mungu amewabariki sana na mengi! Ana uwezo mkubwa wa mali na hana shida kihivyo, ila akikuona wewe maskini umefanikiwa kidogo tuu, na wala hata hujamzidi, anapatwa na hofu na kutetemeka. Ana mengi lakini kidogo chako kinamkosesha amani kabisa. Jitahidi kuepuka kuogopa kupitwa kwani maisha hubadilika pia.*
1.Mtu mmoja aliyejitolea ni bora kuliko watu kumi waliolazimishwa kufanya kazi
2.Anayekula chakula kwakujificha hawezi kuelezea jinsi chakula kilivyokuwa kitamu
3.Kidole kimoja hakitoshi kuosha uso mzima
4.Aliye na kuni nyingi kuliko wewe ana majivu mengi kuliko wewe
unikumbuke leo kwenye sala zako ninapoendelea kuomba msaada wa MUNGU katika changamoto mbali mbali zilizo mbele yangu za maisha.
Francis
Mtumishi wa Mungu