06/08/2024
REHEMA & KWELI ZA BWANA
Kuna mambo 5 yanayompa mtu kutembea chini ya rehema (mercy), neema ( grace) na upendeleo wa kiungu ( divine favor)...
Mungu amejitambulisha kuwa mwenye huruma nyingi
Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
[ And the LORD passed by before him, and proclaimed, The LORD, The LORD God, merciful and gracious, longsuffering, and abundant in goodness and truth, ]
Lakini....
Usiseme Mungu ni wa huruma na rehema hivyo ukawa mjinga kiasi cha kuwa na mwenendo wa kudumu usiopatana na injili ambayo kwayo uliokokewa...
Ingawa Bwana husamehe na ni mwenye huruma ila hawi radhi na wapumbavu siku zote....
Ni Bwana mwenye huruma na rehema nyingi huyu huyu ambaye kwa Manung’uniko aliwazuilia wana wa Yakobo kuiona nchi ya Ahadi akamruhusu Rahabu kahaba badala yake....
Ni Mungu huyu huyu...
Hata hivyo kuna namna nne zinazovuta huruma na rehema za Kimungu juu ya mtu kiasi cha kutoruhusu mkono wake au wa shetani umguse mtu huyo....
1. Jifunze kuungama (confess)
Hii ni hatua ya kwanza na ya muhimu kila mara nafsi yako inapokuhukumu (convict) kuhusu mwenendo fulani usio sawa. Dhamiri ya mtu ni sauti ya mtu wa ndani na itakwambia ukweli siku zote kuliko ukweli anaoweza kukwambia mtu yeyote. Jifunze kumweleza Mungu ukubwa wa kosa lako kinagaubaga bila kulipamba au kulifunika-funika (covering) wala kujitetea.
Hilo ndio maana ya Ungamo. Kutambua kosa lako na kuliungama k**a lilivyo ni hatua ya kwanza ambayo huvuta huruma, rehema, neema, upendeleo na kibali cha kiungu juu ya mtu.
2. Tubu (Repent )
Toba (Repentance) ni kuacha (forsake).
Ni kuamua toka moyoni na kwa nia dhabiti kuacha njia mbaya.
It is an intentional and total change from evil..
Wakati ungamo (confession) mi ukiri wa ulimi, toba ni badiliko ya jumla la kitabia/kimwenendo.
Ikiwa unakiri dhambi ile ile kila siku mbele za Mungu, huo sio udhaifu tena bali kifungo wala hiyo sio toba bali ungamo.
Ni sawa umekiri kuwa unatembea na mme wa Mtu, bado Mungu anakuhesabu kuwa mwasherati na mzinzi hadi utakapokuja mbele zake na kumwambia Bwana nimeacha.
Mungu hahitaji maneno zaidi k**a anavyofurahia kitendo hiki cha mtu kuacha njia zake mbaya...
Kwahiyo
Ungamo + Toba = Rehema + Mafanikio
Mithali 28:13
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
[ He that covereth his sins shall not prosper: but whoso confesseth and forsaketh them shall have mercy.
Sio kuungama tu bali na kuacha kabisa...
Mungu ni rafiki wa watu wanaoungama na kuacha njia zao mbaya kuliko watu wanaojihesabia haki kila kukicha....
Ati Mungu ni rafiki wa Daudi muuaji....
Kuacha njia mbaya ndio toba....
3. Jifunze Kusamehe ( Forgive)
Mungu huwapenda watu wenye huruma na wepesi wa kusamehe...
Usisamehe hutasamehewa...
K**a unataka kuishi maisha ya kibali, rehema na upendeleo wa Mungu, jifunze kuwasamehe ndugu zako hawa wanaokuudhi na kukukosea kila siku...
Msamaha wetu wa kibinadamu huruhusu mtembeo wa rehema na msamaha mkubwa wa kiungu juu yetu....
Mathayo 6:14-15
"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu"
[ For if ye forgive men their trespasses, your heavenly Father will also forgive you: But if ye forgive not men their trespasses, neither will your Father forgive your trespasses. ]
Daudi alimsamehe Sauli wala hakuwalipiza kisasi adui zake wa waziwazi.....
4. Jifunze kumtii Mungu
Isaya 1:19 K**a mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya 1:20 bali k**a mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
[ If ye be willing and obedient, ye shall eat the good of the land: But if ye refuse and rebel, ye shall be devoured with the sword: for the mouth of the LORD hath spoken it]
Utii ni alama muhimu ya mwana wa Mungu.
Ingawa Mungu ni mwenye rehema lakini roho mbaya ( evil spirit) ilivyomwingia Sauli hata asimsikilize Ssmweli nabii wake Mungu alimkataa.
Hivyo hivyo kwa Yuda wa Iskariote..
Mungu anafurahishwa na utii wetu kuliko kazi zetu tunazoita za kumvunia watu...
Anatamani kuvuna moyo wako kabla ya kukutumia kuvuna wengine...
5. Uwe Mnyenyekevu ( Be humble).
Isaya 66:2b
"...lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu"
[..... but to this man will I look, even to him that is poor and of a contrite spirit, and trembleth at my word.]
K**a ilivyo hekima, unyenyekevu ni roho pia na unaweza kwa kiasi fulani 'kujifunza kuwa'. Mungu anawapenda na kuwahurumia mno watu wanyenyekevu kwa neno neno lake wanapolisikia kutoka kwa kinywa cha nabii wake au kutoka kwake.
Mungu huwapenda watu wanaoukubali msalaba na neno k**a ukamilifu wa njia zao kuliko kutegemea akili zao wenyewe.
Watu waliopondokeka mioyo na sio wajuaji wasiotaka kufundishwa na mtu au Bwana...
Hakuna namna rehema za Mungu zitafanya kazi kwa mtu aliyeshupaza shingo yake...
Mithali 29:1 Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.
[ He, that being often reproved hardeneth his neck, shall suddenly be destroyed, and that without remedy.]
Dr. Kazabao Edson
+255763575550