Habari Za Bwana

Habari Za Bwana Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Habari Za Bwana, anthonyjanuary10@gmail. com, Tanza.

22/07/2020

Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao(::2 )heri wenye huzuni maana hao watafarijika ( 3)heri wenye upole maana hao watairithi nchi (4)heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa (5)heri wenye rehema maana hao watapata rehema (6)heri wenye moyo safi maana hao watamwona mungu (7)heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa mungu (8)heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki maana ufalme wa mungu ni wao !!!!!ninyi ni nuru ya uli mwengu ..NI MAANDIKO TOKA MATAHAYO MTAKATIFU5:1:12

26/10/2018

JAMBO LA KWANZA
Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano wako na wazazi wako.
Mwanzo.2:24 anasema, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja”. Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, “Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie”. Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako. Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo – ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako k**a umeoa, na ni mume wako k**a umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako. Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa. Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema, “Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie”. Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia, “your priorities must change” lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao. Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu. Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako. Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana. Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani. Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata k**a atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni, – anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; kwa nini? Kwa sababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake. Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi. Unaweza sasa ukaelewa kwa nini watu wengine ikifika siku ile ya “send off”, yaani ya kum’send’ msichana ‘off’ asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwa sababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine. Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.

03/10/2018

MHUBIR 4:13 Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo

30/09/2018

Mlango 7

1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.Kutweza Kitakatifu
6 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.Omba, Tafuta, Bisha
7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?
10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?
11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?Amri Kuu
12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.Mlango Mwembamba
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.Mti na Matunda Yake
15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.Kuhusu Wanaojihadaa
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.Wasikiao na Watendao
24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

30/09/2018

UFUNUO 19;7

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.}

Naungana na ndugu, jamaa na marafiki wa familia waliopoteza maisha katika ajali ya    azilaze roho za marehem mahali pem...
22/09/2018

Naungana na ndugu, jamaa na marafiki wa familia waliopoteza maisha katika ajali ya azilaze roho za marehem mahali pema pepon Amina

19/09/2018

kumbukumbu la torati : Mlango 11
12 nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.
K**A UNATAKA KUTUNZWA NA BWANA KWANZIA MWANZO WA MWAKA HATA MWISHO SEMA
MACHO YA BWANA UWE JUU YANGU

Msemaji wa Mwisho ni Mungu pekee kwenye maisha yakowanadamu wamesema sana Tangu mwanzo wa maisha Yako Ni maombi yangu kw...
30/08/2018

Msemaji wa Mwisho ni Mungu pekee kwenye maisha yako
wanadamu wamesema sana Tangu mwanzo wa maisha Yako
Ni maombi yangu kwa Mungu aseme sasa juu ya maisha yako
K**A UNAAMINI SEMA
Mungu naomba useme sasa

Mathayo 6:11Utupe leo riziki yetu.Ni ombi ambalo limesaulika kwa wengi lakin ni lamuhimu kwa wote, leo nakukumbusha Mung...
29/08/2018

Mathayo 6:11
Utupe leo riziki yetu.
Ni ombi ambalo limesaulika kwa wengi lakin ni lamuhimu kwa wote,
leo nakukumbusha
Mungu akupe riziki yako ya leo kwajina la YESU KRISTO.

29/08/2018

Usichanganye huduma ya Mungu ndani ya mtumishi na maisha ya kibinadamu ya mtumishi.. Daudi alikua mtumishi WA Mungu Tena Mungu anasema Daudi ni Rafik yake. Lakini Daud aliua mume WA mtu ili amrithi mke wake.. Usichanganye Iman na dhambi ya mtumishi. Rahabu alikua kahaba lakini ndye aliyewahifadhi wapelelezi WA Israel Yeriko. Na Yesu ametoka kwnye ukoo WA Rahabu.. Njia za Mungu sio za mwanadmu. Mungu aliinua vinyonge ili kuvidhoofisha vyenye nguvu.. Nabii Eliya alikua na ujasiri kufanya kazi ya Mungu aliua manabii WA Baali 400 cha hajabu alimuogopa Yezebeli. Mpendwa usiishi maisha ya kiroho Kwa ushuhuda za mwingine ziwe mzuri au mbaya, utachelewa.

29/08/2018

Zaburi 2:3-4
[3]Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
[4]Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

NGOZI CRATER LAKE. (volcanic lake) Also known as the serpent lake, 8km long and 4km wide. Acaldera Crater which was late...
28/08/2018

NGOZI CRATER LAKE.
(volcanic lake)
Also known as the serpent lake, 8km long and 4km wide. Acaldera Crater which was later filled by the Ngozi crater lake, dating millions years back. Also known to be home of monster.

 !!!!tunda ili lina patikana Kwa wingi Wilaya ya Kyela Mkoa Wa Mbeya
28/08/2018

!!!!tunda ili lina patikana Kwa wingi Wilaya ya Kyela Mkoa Wa Mbeya

LIPARAMBA:PORI LILILOPO UKANDA MAARUFU DUNIANI WA MIOMBOpori la Akiba la Liparamba lipo katika ukanda wa wa misitu maaru...
28/08/2018

LIPARAMBA:PORI LILILOPO UKANDA MAARUFU DUNIANI WA MIOMBO
pori la Akiba la Liparamba lipo katika ukanda wa wa misitu maarufu duniani ya miombo woodland.Pori linakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 60,00 kulingana na utafiti ambao ulifanywa mwaka 2011.
Pori hilo linapita katika wilaya za Songea,Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma, lilikabidhiwa rasmi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya usimamizi wa Idara ya Wanyamapori serikani Juni 5 mwaka 2006.Pori lina ukubwa wa kilometa za mraba 571 likiwa na eneo la kilometa za mraba 11,396.
Kutokana na ukubwa wa misitu mizito minene iliyopo katika pori hilo inachangia kupunguza hewa ukaa(CO2).Liparamba ni eneo muhimu katika mchakato wa (Carbon sink) ambao hupokea mvua za kutosha kwa msimu mmoja tu kwa mwaka.Miongoni mwa vivutio adimu katika pori hili ni uoto wa asili, zikiwemo aina 60 za miombo,nyasi adimu aina 35,aina 80 za ndege na wanyama wa aina mbalimbali .

Address

Anthonyjanuary10@gmail. Com
Tanza
225

Telephone

+255 767 438 502

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari Za Bwana posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Habari Za Bwana:

Share