12/03/2024
NYAKATI NGUMU zitakutenga na watu ULIOWAZOEA.
Sio kila mtu anaweza KUSIMAMA na wewe Kwenye NYAKATI ZAKO NGUMU.
Kuna aina fulani ya watu ambao watakuwa na wewe kwenye RAHA TU...
..Ila kwenye MAGUMU HAUTAWAONA.
Kuna watu ukipata AIBU hawatakuwa tayari “Kujiidentify” na wewe...
..yaani watajifanya K**a HAWAKUJUI KABISA.
Ndio maisha yalivyo, nyakati ngumu zinakusaidia sana KUCHUJA aina ya watu kwenye maisha.
Inakupa hekima ya kujua NAFASI uliyonayo Kwenye MIOYO YA WATU.
Hii ndio maana, watu wengi WAKISHAVUKA kutoka kwenye NYAKATI NGUMU...
..Utashangaa wamepata aina nyingine ya MARAFIKI.
Sio kila RAFIKI uliyenaye ATAKUWA na wewe Kwenye Nyakati zako ngumu...
..JIANDAE KISAIKOLOJIA.
K**a umejifunza kitu comment neno "NIMEJIFUNZA KITU"
See You At The Top
Joel Arthur Nanauka