Ngorongoro Conservation Area Authority

Ngorongoro Conservation Area Authority A Mixed World Heritage Site, Man and Biosphere Reserve and UNESCO Global Geopark. The Eighth wonder of the World.
(3)

Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) is a parastatal organisation mandated to manage Ngorongoro Conservation Area (NCA) that was established in 1959 by the Ngorongoro Area Ordinance No. 14 of 1959 and revised as the Ngorongoro Conservation Area Act (Cap. 284 R.E. 2002). The three main functions of NCAA are:-
i) To conserve and develop the natural resources in the conservation area. ii) To

safeguard and promote the interests of Maasai citizens of the United Republic engaged in cattle ranching and dairy industry within the conservation area. iii) To promote tourism in the conservation area and to provide and encourage the provision of facilities necessary or expedient for the promotion of tourism.

TUMEAMUA KUHAMA KWA HIARI NDANI YA HIFADHI KWENDA MSOMERA- WANANCHI NGORONGORO Na Philomea Mbirika, NCAA.Jumla ya wananc...
19/12/2024

TUMEAMUA KUHAMA KWA HIARI NDANI YA HIFADHI KWENDA MSOMERA- WANANCHI NGORONGORO

Na Philomea Mbirika, NCAA.

Jumla ya wananchi 97 waliokubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Kwenda Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Tanga, wametoa wito kwa wananchi wenzao waliobaki ndani ya hifadhi kujiandikisha ili wapate uhuru na fursa ya kuboresha maisha yao nje ya Hifadhi na kuepuka hatari ya kuishi na wanyama wakali katika eneo moja.

Wito huo umetolewa leo tarehe 19 Desemba 2024 na wawakilishi wa wananchi hao ambapo kundi la 21 la awamu ya pili lenye kaya 23, watu 97 na mifugo 196 limehama kwa hiari ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera na maeneo Mengine waliyochagua wenyewe.

Bw. Daudi Melubo kutoka kijiji cha Kayapus ambaye ni mmoja wa wananchi waliohama leo amesema yeye na familia yake waliamua kufanya maamuzi ya kuhama ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na kutokua na uhuru wa kujiendeleza kiuchumi kutokana na sheria za uhifadhi.

“Mimi nimeamua kuhama kwa hiyari yangu kwenda Msomera kwa sababu huko kuna uhuru wa kujiendeleza, nitajenga nyumba, nitamiliki ardhi, watoto wangu wataenda shule bila hofu ya mnyama na hakuna sheria k**a hifadhini, nawashauri ndugu zangu ambao bado hawajajiandikisha kuhama kwa hiari na watapata fursa ya kuendeleza na kuboresha maisha yao” Alisema Daudi

Kwa upande wake, Bi. Naishiye Sembeta alieleza kuwa;
“Sisi wanawake tumekuwa tukitembea umbali mrefu kwenda kutafuta kuni porini huku tukihatarisha maisha yetu, ila sasa tunahamia Msomera na tunaamini maisha yetu yatabadilika na kuwa bora zaidi” alisema Naishiye

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo, Meneja wa mradi Afisa uhifadhi Mkuu Flora Asey amesema kuwa hadi kufikia leo tarehe 19/12/2024 jumla ya kaya 1,678 zenye watu 10,073 na mifugo 40,593 zimekwisha hama ndani ya Hifadhi kuelekea Msomera na wengine kwenye maeneo waliyochaguwa wenyewe.

Assey alisisitiza kuwa kwa sasa utaratibu uliopo ni kuhakikisha kuwa zoezi la uandikishaji, tathmini ya maendelezo na uhamishaji vinaenda sambamba ili kuhakikisha kila mwananchi anapojiandikisha anatumia muda mfupi kuhama ndani ya hifadhi kwenda eneo alilochagua

Zoezi la kuhama kwa hiari ndani ya hifadhi ya Ngorongoro linaendelea ambapo adhma ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kuwa wananchi hao wanapata fursa ya kuishi katika maeneo salama yenye huduma zote muhimu za kijamii kwa ajili ya maendelea ya wananchi hao.

Jiraniiiii!!! Mwambie jirani amwambie jirani yake, msimu huu wa sikukuu ni eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Njooni mjionee...
17/12/2024

Jiraniiiii!!! Mwambie jirani amwambie jirani yake, msimu huu wa sikukuu ni eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Njooni mjionee uzuri wa maajabu ya asili na mandhari ya kipekee. Ngorongoro inakuita jirani!




HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGOROTarehe 15 Desemba 2024 Kreta ya Ngorongoro imepambwa na tukio adhimu na...
16/12/2024

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

Tarehe 15 Desemba 2024 Kreta ya Ngorongoro imepambwa na tukio adhimu na la kihistoria la maharusi wa Kitanzania kufunga ndoa ndani ya Hifadhi huku hao wakipunga upepo mwanana kwenye mazingira asilia yaliyozungukwa na wanyama mbalimbali wakiwemo Big 5.

Bw. Kelvin Mwakaleke na mkewe
Jackline Nyalu wamefunga Ndoa ndani ya Kreta ya Ngorongoro wakisindikizwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki huku wakishuhudiwa na macho ya Wanyama mbalimbali wakiwemo Simba, Faru, Tembo, Nyati, Chui, Pundamilia, Nyumbu, Thomson Gazelle, ambao wamekuwa mashuhuda wa tukio hilo lililofanyika pembeni mwa bwawa maarufu la Ngoitoktok wakati huo Viboko wakinogesha shughuli kwa kuogelea.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mariam Kobelo anayesimamia huduma za Utalii na Masoko NCAA ameeleza kuwa “Leo ni siku ya furaha na ya kipekee isiyosahaulika, tumeshuhudia tukio adhimu na akramu lenye baraka za Mungu kwa maharusi hawa kufunga ndoa kwenye bustani ya Eden (Ngorongoro Crater).

Kufunga ndoa ndani ya hifadhi ni fursa muhimu katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro hali inayoamsha ari kwa watalii wa ndani kuongezeka na kuchangia mapato ya Serikali.

Akielezea tukio hilo huku Bwana harusi Kelvin Mwakaleke akiwa na mkewe Jackline ameeleza kuwa kufunga ndoa ndani ya hifadhi ilikiwa ndoto yake ambayo hatimae imetimia.

“Nilimuomba Mungu kuniongoza kufanikisha tukio hili, kufunga ndoa kreta ni uzoefu ambao siwezi kuusahau, ni eneo lenye vivutio vya kila aina kwa mtu yoyote kutembelea, lina uzuri wa asili wanyama wengi na uoto wa asili uliohifadhiwa vema, mimi, mke wangu na ndugu wachache tuliounganika hapa tutakuwa mabalozi wa kuitangaza hifadhi ya Ngorongoro” alisema Bw. Mwakaleke.






Sikukuu ni Ngorongoro!Furahia msimu wa sikukuu katika uzuri wa asili wa Hifadhi ya Ngorongoro. Tembelea vivutio vya kipe...
15/12/2024

Sikukuu ni Ngorongoro!
Furahia msimu wa sikukuu katika uzuri wa asili wa Hifadhi ya Ngorongoro. Tembelea vivutio vya kipekee, shuhudia wanyama pori, na utengeneze kumbukumbu zisizosahaulika. Hapa, kila hatua ni safari ya ajabu. Karibu Ngorongoro!




UNESCO YARIDHISHWA NA HIFADHI YA JIOLOJIA YA NGORONGORO LENGAI.Kikao cha Wajumbe wa Baraza la UNESCO la Jiopaki kilichof...
14/12/2024

UNESCO YARIDHISHWA NA HIFADHI YA JIOLOJIA YA NGORONGORO LENGAI.

Kikao cha Wajumbe wa Baraza la UNESCO la Jiopaki kilichofanyika tarehe 10 Desemba, 2024 kwa njia ya mtandao kimeridhishwa na shughuli za uhifadhi wa Jiolojia ya Ngorongoro Lengai ambapo NCAA imewakilishwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Dkt. Agness Gidna.

Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko kusini mwa jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai (Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark) ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imepata kadi ya kijani (GREEN CARD) k**a ishara ya umahiri katika uhifadhi na utangazaji wa eneo lenye hadhi ya hifadhi ya Jiolojia (Geopark) kwa kufuata masharti na miongozo ya UNESCO.

Kwa utaratibu wa UNESCO, maeneo yenye hadhi za Jiolojia (Geopark) za UNESCO zinakaguliwa kwa kina kila baada ya miaka minne kwa ajili ya kupima na kuona ufanisi na ubora kupitia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika maeneo hayo kwa kufuata vigezo vilivyoainishwa na UNESCO.

Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (Geopark) inayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongroro ilipata hadhi ya kutambuliwa na UNESCO Global Geoparks mwaka 2018, kutambuliwa huko kuliifanya kuwa Jiopaki pekee kusini mwa jangwa la Sahara na jiopaki ya pili katika bara la Afrika ikitanguliwa na M’Goun geopark ya nchini Morocco.

Katika tathmini na ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka UNESCO mwaka 2022, hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro Lengai ilipata kadi ya njano (Yellow Card), ambapo kwa miongozo ya UNESCO Ngorongoro Lengai ilitakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza ndani ya miaka miwili ili kulinda hadhi iliyopewa mwaka 2018.

*UNESCO YARIDHISHWA NA HIFADHI YA JIOLOJIA YA NGORONGORO LENGAI.*  *YATOA KADI YA KIJANI K**A ISHARA YA UMAHIRI KATIKA U...
14/12/2024

*UNESCO YARIDHISHWA NA HIFADHI YA JIOLOJIA YA NGORONGORO LENGAI.*

*YATOA KADI YA KIJANI K**A ISHARA YA UMAHIRI KATIKA UHIFADHI NA UTANGAZAJI WA ENEO LENYE HADHI YA HIFADHI YA JIOLOJIA (GEOPARK)*

Na Kassim Nyaki, NCAA.

Kikao cha Wajumbe wa Baraza la UNESCO la Jiopaki kilichofanyika tarehe 10 Desemba, 2024 kwa njia ya mtandao kimeridhishwa na shughuli za uhifadhi wa Jiolojia ya Ngorongoro Lengai ambapo NCAA imewakilishwa na Afisa Uhifadhi Mkuu Dkt. Agness Gidna.

Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko kusini mwa jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai (Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark) ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imepata kadi ya kijani (GREEN CARD) k**a ishara ya umahiri katika uhifadhi na utangazaji wa eneo lenye hadhi ya hifadhi ya Jiolojia (Geopark) kwa kufuata masharti na miongozo ya UNESCO.

Kwa utaratibu wa UNESCO, maeneo yenye hadhi za Jiolojia (Geopark) za UNESCO zinakaguliwa kwa kina kila baada ya miaka minne kwa ajili ya kupima na kuona ufanisi na ubora kupitia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika maeneo hayo kwa kufuata vigezo vilivyoainishwa na UNESCO.

Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (Geopark) inayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongroro ilipata hadhi ya kutambuliwa na UNESCO Global Geoparks mwaka 2018, kutambuliwa huko kuliifanya kuwa Jiopaki pekee kusini mwa jangwa la Sahara na jiopaki ya pili katika bara la Afrika ikitanguliwa na M'Goun geopark ya nchini Morocco.

Katika tathmini na ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka UNESCO mwaka 2022, hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro Lengai ilipata kadi ya njano (Yellow Card), ambapo kwa miongozo ya UNESCO Ngorongoro Lengai ilitakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza ndani ya miaka miwili ili kulinda hadhi iliyopewa mwaka 2018.

Jitihada za serikali kupitia NCAA hasa katika uimarishaji wa shughuli za uhifadhi, Ulinzi, kutangaza, kufuata masharti na miongozo ya UNESCO katika kulinda hadhi ya eneo hilo ili kuendelea kuwa Hifadhi ya Jiolojia inayotambulika k**a “Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark” zilizaa matunda baada ya timu ya UNESCO iliyokuja mwezi julai, 2024 kufanya uthibitishaji upya (Revalidation) ambapo waliridhika na hatua zilizofanywa na Serikali katika kufuata ,miongozo ya UNESCO katika eneo hilo.

Faida ambazo Tanzania itazipata kwa kuwa na kadi ya kijani (GREEN CARD) ni pamoja na kuongezeka kwa muonekano chanya wa uhifadhi kwa nchi ya Tanzania kimataifa, kuongezeka kwa idadi ya watalii na watafiti watakaotembelea nchi ya Tanzania kwa Shughuli mbalimbali.

Faida zingine ambazo nchi inazipata ni pamoja na kupanua wigo wa mashirikiano ya kimataifa katika sekta ya uhifadhi na utalii wa hifadhi ya Jiolojia (Geopark) pamoja na kuongeza fursa ya kuongeza vivutio vingi vya utalii na hasa utalii wa miamba.

🚨BREAKING NEWS🚨Ngorongoro Lengai has maintained the quality of UNESCO Global Geoparks after revalidation and recommendat...
13/12/2024

🚨BREAKING NEWS🚨

Ngorongoro Lengai has maintained the quality of UNESCO Global Geoparks after revalidation and recommendation of the UNESCO Global Geopark Council.




The Zinj Skull serves as a powerful symbol in the story of human evolution, having been discovered in Ngorongoro in 1959...
13/12/2024

The Zinj Skull serves as a powerful symbol in the story of human evolution, having been discovered in Ngorongoro in 1959. Understanding the significance of the Zinj Skull is crucial, as it demonstrates how perseverance and dedication can illuminate the path of discovery, inspiring future generations to explore the mysteries of our origins.



Lions are part of Africa's "Big Five," representing the most iconic wildlife. These majestic animals symbolize strength ...
12/12/2024

Lions are part of Africa's "Big Five," representing the most iconic wildlife. These majestic animals symbolize strength and pose unique challenges for hunters, attracting wildlife enthusiasts and adventure seekers. Encountering lions in their natural habitat is an unforgettable adventure!



Lions are part of Africa’s “Big Five,” representing the most iconic wildlife. These majestic animals symbolize strength ...
12/12/2024

Lions are part of Africa’s “Big Five,” representing the most iconic wildlife. These majestic animals symbolize strength and pose unique challenges for hunters, attracting wildlife enthusiasts and adventure seekers. Encountering lions in their natural habitat is an unforgettable adventure!



Wildebeests are famous for their annual migration (Great Migration), where thousands of them travel in large herds in se...
11/12/2024

Wildebeests are famous for their annual migration (Great Migration), where thousands of them travel in large herds in search of pasture and water.

THE WILD IS CALLING, BOOK NOW!!
10/12/2024

THE WILD IS CALLING, BOOK NOW!!



MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU, NCAA YAGAWA MICHE YA MITI 2,000 KWA JWTZ.Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanza...
09/12/2024

MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU, NCAA YAGAWA MICHE YA MITI 2,000 KWA JWTZ.

Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa miche ya miti 2,000 kwa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) 303 KV, Arusha ili kuweza kuboresha utunzaji wa mazingira.

Miti hiyo iliyotolewa kwenye kitalu cha miti kinachosimamiwa na NCAA, inatarajiwa kupandwa na JWTZ kwenye maeneo mbalimbali Wilayani Monduli, Arusha.

Maadhimisho ya siku hii ya uhuru hufanyika kila mwaka tarehe 9 Disemba, ambayo kwa mwaka huu ni maadhimisho ya Miaka 63 tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanzania bara ikiwa na kauli mbiu isemayo “Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa Maendeleo yetu”.

THE WILD IS CALLING, BOOK NOW!!
06/12/2024

THE WILD IS CALLING, BOOK NOW!!

05/12/2024

A Mixed World Heritage Site, Man and Biosphere Reserve and UNESCO Global Geopark. The Eighth wonder o

VIJANA WA ACTION ROLLERS MTAA KWA MTAA KUTANGAZA KAMPENI YA UTALII KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU.Na Kassim Nyaki-NCAAKufuati...
05/12/2024

VIJANA WA ACTION ROLLERS MTAA KWA MTAA KUTANGAZA KAMPENI YA UTALII KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU.

Na Kassim Nyaki-NCAA

Kufuatia Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kuzindua msimu ya kampeni ya kuhamasisha utalii kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka vijana wa Action Rollers Skates wako katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha kutangaza kampeni hiyo.

Vijana hao ni sehemu ya njia mbalimbali zinazotumiwa na NCAA kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kutumia mabango yenye vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, kutembea na mabango yenye vifurushi vya gharama za kuingia hifadhini na kuvaa sare za tisheti zenye ujumbe wa kuhamasisha kampeni hiyo kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo ni Merry and Wild; Ngorongoro Awaits” ambayo imeanza tarehe 4 Desemba, 2024 hadi tarehe 4 Januari, 2025 imegawanyika katika vifurushi vya aina tatu k**a ifuatavyo;

Kifurushi cha FARU chenye gharama ya Shilingi 450,000 kwa mtu, ambapo gharama hiyo inahusisha utalii kwa siku mbili (02) hifadhi ya Ngorongoro, kiingilio, Malazi, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha na ambapo safari itakuwa tarehe 24-25 Desembaa 2024.

Kifurushi cha Pili ni TEMBO chenye gharama ya Shilingi 130,000 kwa mtu, kifurushi hiki kinahusisha utalii kwa siku moja (01) Day trip Ngorongoro na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha ambapo safari itakuwa tarehe 25 desemba, 2024

Kifurushi cha tatu ni CHUI chenye gharama ya Shilingi 85,000 kwa mtu na gharama hiyo itajumuisha Usafiri wa basi, kiingilio, Chakula, muongoza watalii na huduma ya picha ambapo safari tarehe 29 Desemba, 2024.

Katika utekelezaji wa Kampeni hiyo NCAA inashirikiana na kampuni ya Tanzania Smile Safaris ambapo watanzania wanaopenda kunufaika na kampeni hiyo wanakaribishwa kupiga simu kwa namba 0755 559013 ili kuweka nafasi (booking).

Alhamisi ya Kumbukizi (TBT)
05/12/2024

Alhamisi ya Kumbukizi (TBT)

Address

Ngorongoro Crater
Arusha
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ngorongoro Conservation Area Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ngorongoro Conservation Area Authority:

Videos

Share

Our Story

Ngorongoro Conservationa Area Authority (NCAA) is a parastatal organisation madated to manage Ngorongoro Conservation Area (NCA) that was established in 1959 by the Ngorongoro Area Ordinance No. 14 of 1959 and revised as the Ngorongoro Conservation Area Act (Cap. 284 R.E. 2002). The three main functions of NCAA are:- i) To conserve and develop the natural resources in the conservation area. ii) To safeguard and promote the interests of Maasai citizens of the United Republic engaged in cattle ranching and dairy industry within the conservation area. iii) To promote tourism in the conservation area and to provide and encourage the provision of facilities necessary or expedient for the promotion of tourism.