06/12/2019
MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU BUSTANI YA MUNGU- HIFADHI YA KITULO
1.Hifadhi ya Taifa Kitulo ndiyo eneo pekee Tanzania lenye ndege aina ya tandawala machaka (Denhams Bustard) wenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
2.Hifadhi hiyo inayopita katika mikoa ya Mbeya na Njombe ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 2005 ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, msitu wa Livingstone na bonde la Numbi.
3.Kitulo ina ukubwa wa kilometa za mraba 442. Awali ilijulikana k**a Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredirick Elton kupita eneo hilo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hilo kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
4. Ndege aina ya tandawili machaka hawapatikani sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania zaidi ya Kitulo.
5.hifadhi hiyo ndiyo eneo pekee ambalo ndege hao hutaga mayai na kuzaliana kwa wingi kabla ya kusafiri kwenda mabara mengine.
6.Utafiti unaonyesha kuna ndege aina ya tandawili machaka ambao waliwekwa alama walipokuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na baadaye kuonekana wakiwa na alama zao katika hifadhi moja Australia.
7. Ndege hao wamekuwa na tabia katika msimu fulani kuruka na kufika katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kwa ajili ya kutaga mayai na kuangua vifaranga kutokana na mazingira ya hifadhi hiyo kuonekana kuwa ni mahali pekee duniani penye hali ya hewa rafiki kwa ndege hao kuzaliana. Hivyo baada ya kutaga mayai, kuangua vifaranga na ndege kukua, huruka na kwenda mabara mengine duniani.
8.Utafiti umebaini kuwa katika Hifadhi ya Kitulo ndege aina ya abdims stock, denhams (tandawili machaka) na blue swallow ambao wametoka Afrika Kaskazini, Afrika Kusini, Australia na Ulaya wanaitumia Hifadhi ya Kitulo k**a makazi yao katika misimu tofauti.
9.Hifadhi ya Kitulo pia inasifika kwa kuwa na zaidi ya aina 40 za maua mbalimbali ambayo hayapatikani sehemu nyingine duniani.
10. Muda mzuri kutembela; kuona maua- Dec-April, Sept-Nov ni muda mzuri kwa kupanda vilima, June- Aug ni baridi.
Kitulo National Park
Locals refer to the Kitulo Plateau as Bustani ya Mungu – The Garden of God – while botanists have dubbed it the Serengeti of Flowers, host to ‘one of the great floral spectacles of the world’. And Kitulo is indeed a rare botanical marvel, home to a full 350 species of vascular plants, including 45 varieties of terrestrial orchid, which erupt into a riotous wildflower display of breathtaking scale and diversity during the main rainy season of late November to April.
Kitulo National Park stands alone, boasting of being the only tourist attractive site in the continent offering floristic visits than the traditional wildlife photographic holidays which most tourists to Tanzania are used to experience
Best Time To Visit
- Wildflower display peaks between December and April.
- The sunnier months of September to November are more comfortable for hiking but less rewarding to botanists.
- Conditions are cold and foggy from June to August.