SMB Consulting

SMB Consulting Ndoto yako ya kufika ughaibuni inatimia hivi punde.

26/08/2024

Mitaa ya Korea nyakati za usiku.

03/08/2024

Hatusimuliwi, tunafika kujionea.

Nikiwa pearson international Airport.

14/07/2024

Union Bus Station.

Hiki ni kituo kikubwa cha mabus na treni ziendazo nje ya Mji wa Toronto hapa Canada.

Je kinafanana na kituo cha mji uliopo?

K**a unatata kuhamia Canada wewe na familia yako na una bachelor degree karibu ofisini nikupe ushauri. Kwa sasa nafasi z...
08/06/2024

K**a unatata kuhamia Canada wewe na familia yako na una bachelor degree karibu ofisini nikupe ushauri. Kwa sasa nafasi za kuonana nami zipo kuanzia tar 20-30 June. Baada ya hapo nirarejea Canada.

Consultation fee ni $50.

05/05/2024

Mzazi hua unazingatia nini wakati unapomtafutia mwanao chuo nje ya nchi? Huu hapa ushauri wangu usikilize kwa makini

04/05/2024

K**a ulikua na mpango wa kuja Canada kutafuta MAISHA jitahidi ufanye Application ya VISA kabla ya mwezi september mwaka huu. Sikiliza kwa makini maelezo yangu kwenye video

03/05/2024

Kabla hujafanya maamuzi ya nchi ya kwenda kusoma kati ya Canada na Marekani nisikilize kwa umakini

Tokea nije Canada nimebadili mtizamo kiasi kikubwa kuhusu kusoma nje ya nchi, nimetamani miaka yangu 6 niliyoitumia kuso...
03/05/2024

Tokea nije Canada nimebadili mtizamo kiasi kikubwa kuhusu kusoma nje ya nchi, nimetamani miaka yangu 6 niliyoitumia kusoma Uturuki ningeitumia hapa Canada au Marekani.

Wewe K**a ni mzazi unayemtakia mwanao mfanikio usifanye makosa haya unapomtafutia mwanao chuo nje ya nchi.

Bonya Learn More kufahamu zaidi.

20/04/2024

Facebook ina watu OG sana.

Nimeandika kitabu hiki cha CHECKLIST ili kikupe muongozo wa kukagua maeneo sita muhimu pindi biashara yako itakapoyumba....
25/05/2023

Nimeandika kitabu hiki cha CHECKLIST ili kikupe muongozo wa kukagua maeneo sita muhimu pindi biashara yako itakapoyumba.

Kitabu hiki chenye thamani ya Tsh 10,000 Leo utakipata kwa Tsh 3,000 TU (OKOA 7,000)

Na K**a utalipia sasa hivi utajipatia BONUS MBILI

BONUS ya Kwanza ni kitabu changu kingine cha Side Hustle Blueprint kitachokuelekeza njia rahisi ya kutengeneza kipato cha ziada.

BONUS ya Pili ni Course yangu ya Ujasiramali Taarifa Jinsi ya kutumia Smartphone yako kutengeneza Kipato Bila kutoka Chumbani kwako.

OFA Hii ni Kwa Watu 20 Tu Wa Mwanzo kulipia.

Bonyewza Button ya Kuja WhatsApp hapo Chini nikupe namba ya kulipia.

17/05/2023

Huyu Ndiye Mteja Aliyenipa Wakati Mgumu Tokea Nianze Kutoa Huduma za Consultation Kwa Biashara

RT somo lifike kwa wengi…

Ilikua ni siku ya Alkhamis wiki iliyopita, nikiwa ofisini naandaa presentation kwa ajili ya kikao na mteja wangu

Ndipo ghafla..

Simu yangu ikaita, kuishika naona namba iliyokua ikinipigia ilikuwa ngeni na yenye namba namba zisizo za kawaida

Ile kupokea..

Ikaskika sauti ya mmama wa makamo akionekana amechoka na mwenye huzuni kubwa

Mara tu alipojitambulisha akaniambia amepewa namba yangu na rafiki yangu aitwaye Rama aliyekutana nae kwenye CEOs roundtable iliyofanyika wiki mbili zilizopita

alinieleza..

Changamoto yake kubwa ni kwamba, biashara yake ilikua haimletei matokeo anayotaka licha ya kila kitu kuonekana kipo sawa kwenye macho yake

Huduma anayotoa ilionekana kuwa na demand sokoni na alikua na nafasi kubwa ya kufanya vizuri

Baada ya kusikiliza..

maelezo yake na kumuuliza maswali kadhaa nilimuomba anipe muda nilichambue suala lake kisha nimree baada ya siku 2 kwani kwa muda ule na maelezo aliyonipatia hata mimi niliona kila kitu kipo sawa.

Kwanini alikosa matokeo?

Kesho yake yani siku ya ijumaa ndipo nilipolazimika kuyarejea makablasha yangu “my underground notes” mapema asubuhi midaa ya saa mbili mara tu nilipoingia ofisini huku nikijiuliza k**a kuna kitu kilinipita wakati nikiwa shuleni

Na hichi ndicho kilichotokea

Baada ya takriban lisaa limoja na dakika arobaini ndipo nilipoanza kupata mwangaza wa kilichopelekea apate matokeo hafifu.

Na nilipoazama zaidi kwenye material

Ndipo nikakutana na case study ya ya Kampuni ya Kodak na Blockbuster na jinsi zilivyofeli sokon licha ya kuwa vinara kwenye masoko yao kwa muda mrefu

Ile namaliza tu kusoma case study yao tu

Chini ya file la kaki nakakutana na kikaratasi cheupe kilichokunjwa vizuri kwa juu kina maneno yaliyoadnikwa kwa wino mwekundu yanayosomeka “your customers are human beings” na hapo ndipo mchezo ulipoisha.

Ndani ya karatasi ile nilikua nimeandika case study ya kampuni ya Cocacola kwenye kampeni yao ya mwaka 2011 waliyoipa jina la “Share a coke” iliyowapa mafanikio makubwa sokoni

Katika kampeni hiyo kampuni ya Cocacola ilichapisha majina maarufu katika nchi husika na ya kuweka kwenye chupa za soda ya Cocacola sehemu ilikopaswa kuwepo logo yao

Kampeni ile ilihamasisha wateja wanunue soda zenye majina yao na zenye majina ya watu wanaowapenda ili zinunuliwe kwa wingi

Hiyo ilikua ni mbinu ya kujibrand k**a Soda inayojali wateja wake na hivyo kutengeneza muunganiko wa nguvu kihisia baina yao na wateja. Ilikua ni experience ya kipekee kwa wateja kununua soda zenye majina yao na ya wale wanaowapenda.

Na ndani ya mwaka huohuo mauzo yao katika nchi ya Marekani yaliongezeza kwa zaidi ya asilimia 7

Mteja wangu X niliyezungumza nae kwenye simu kampuni yake ilishindwa kutengeneza muunganiko wa kihisia kwa walengwa wao sokoni. Kwa lugha nyingine ilikua imefeli kwenye eneo la Branding.

Eneo ambalo si rahisi kuonekana kwakua ni kitu ambacho hakishikiki. Branding imebeba mafanikio ya kampuni maarufu nyingi duniani ikwemo Cocacola na Apple.

Pengine ulishawahi kuskia neno Branding ukadhani linaamanisha logo au rangi, hapana. Brand ni kitu kisichoonekana, ni experience anayobaki nayo mteja pale ambao product yako haipo.

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kuhakikisha unatengeneza Brand inayowependwa na wateja wako na kuwafanya waendelee kutumia bidhaa zako.

Miongoni mwa mambo hayo ni kuwaelewa wateja wako nje ndani na kutengeneza jumbe mbalimbali ambazo zinazoiunganisha biashara yako na wao.

Watu wanatakiwa wajione kwenye biashara yako kabla ya kutumia bidhaa zako.

Je biashara yako imefanikiwa kutengeneza muunganiko wa kihisia wateja wako?

Je biashara yako inaacha experience gani kwa mteja baada ya mteja kutumia bidhaa yako?

Kumbuka wateja ni wanadamu wenye hisia na mapenzi. Cheza na hisia zao.

Leo kwa mara nyingine tena natoa BURE kitabu changu cha "Maeneo Sita Muhimu ya Kukagua Pindi Biashara yako Inapoyumba"Ki...
15/05/2023

Leo kwa mara nyingine tena natoa BURE kitabu changu cha

"Maeneo Sita Muhimu ya Kukagua Pindi Biashara yako Inapoyumba"

Kitabu hiki kitakusaidia kuitazama biashara yako k**a mfumo uliotengenezwa na vimifumo vidogo vidogo amapo utajifunza jinsi ya kutatua changamoto ya kibiashara haraka ili irudi katika ufanisi wake wa kukuzalishia mapato.

Infanyakazi katika biashara zote.

Nitawapa watu 30 BURE Leo.

Bonya Button ya WhatsApp uje nikupatie.

Hii Ndio Kiki ya Hatari Zaidi Kuwahi Kutengenezwa  DunianiMwanaume mmoja raia wa Australia  ajirusha akiwa kwenye anga l...
15/05/2023

Hii Ndio Kiki ya Hatari Zaidi Kuwahi Kutengenezwa Duniani

Mwanaume mmoja raia wa Australia ajirusha akiwa kwenye anga la urefu wa kilomita 39 kutoka duniani…

Tukio hilo lilitokea October 12 mwaka 2012 ambalo lilirushwa mubashara katika vyombo vya habari dunaini kote na ilichukua takribani dakika 10.

Kwa mara ya kwanza nilipoona video ile nilidhani ni mwanasayansi wa anga akirejea duniani kutokea International Space Station

Kumbe alikua ni mwanamichezo ya kujirusha angani yani Skydiver anayeitwa Felix Baumgartner

Tukio lile lilichukua miaka kuandaliwa na ilimchukua Felix miezi kadhaa ya kufanya mafunzo. Pamoja na consideration zote zilizofanyika bado kulikua na risk kubwa ya bwana Felix kupoteza uhai lakini mwanaume huyu alikubali kuchukua risk

Mfano, baada ya kujirusha aliweza kufikia kasi ya Kilomita 1357 kwa saa (Supersonic) ambayo ilimfanya kuwa binadamu wa kwanza kwenda kasi bila msaada wowote wa kivifaa kushinda kasi ya sauti ambayo husafiri kwa kasi ya Kilomita 1225 kwa saa

Kwa kasi hiyo kulikua kuna uwezekano mkubwa Felix apotelee angani kwani friction yake na hewa ingeweza kupelekea moto na kumfanya aungue na majivu yake yapotelee angani

Hata Astranaunt wa sasa wakiwa wanarudi kutokea ISS katika hatua wanayoihofia zaidi ni pale wanapoingia kwenye atmosphere ya dunia ambako kuna uwezekano mkubwa chombo chao kuungua kutoakana na msuguano mkali wa chumbo na hewa. Rejea Columbia Disaster.

Wakati nikiendelea kutazama tukio lile nilisema kimoyo moyo huku nikibaki mdomo wazi kwa lipi hasa hadi kufikia kuchukua risk kiasi kile!

Nilichokua sikijui ni kwamba nyuma ya tukio lile ilikuwepo kampuni ya vinywaji vya nguvu maarufu duniani inayojulikana kwa jina la Red Bull ambayo inasifika kwa kudhamini michezo ya hatari duniani

RedBull iliwekeza pesa nyingi kufanikisha tukio hilo la kihistoria kuwahi kutokea ulimwenguni lililoipa kampuni hiyo kiki ya nguvu sokoni na kuiongezea heshima katika soko la energy drink.

Lengo kuu la mission nzima ilikua kuongeza awareness ya brand yao kupitia kusisitiza core values za kampuni ya Red Bull ambazo ni “adventure, excitement and pushing the limits of what’s possible”.

Ni misingi inayoifanya Red Bull iendelee kuwa kinara katika soko la Energy Drinks duniani na kwa wapenzi wa michezo ya hatari

Hapa tunapata somo la kwa jinsi gani ni umuhimu kwa brands kusimamia misingi yao na kutengeneza matukio ambayo yafanya fans wao wajiconnect zaidi na brands zao.

Je brand yako ina misingi gani na umefanya kampeni gani kujiconnect na fans wa brand yako?

Raia Waandamana Baada ya Kampuni ya Kinywaji Wanachokipenda Kubadilisha LadhaApril 23 1985 Ndio Siku itayoendelea kukumb...
14/05/2023

Raia Waandamana Baada ya Kampuni ya Kinywaji Wanachokipenda Kubadilisha Ladha

April 23 1985 Ndio Siku itayoendelea kukumbukwa daima kwenye historia ya soko la vinywaji baridi duniani

Hii ni kutokana na kosa la karne lilifanywa na Kampuni Maarufu ya vinjwaji Duniani

Ni kampuni gani?

Kilitokea nini ?

Walijifunza nini?

Somo hadi mwisho ujifunze.

Mnamo miaka ya 1970 kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola ilikutana na upinzani mkali sokoni kutoka kampuni ya Pepsi

Kampuni ya pepsi ilikua ikiffanya tafiti sokoni ya kujua ni ladha ipi inayopendwa zaidi kati ya Pepsi na Cocacola kwa kuwapa wateja waonje bila wao kujua wanaonja soda gani

Baada ya pespi kujiridhisha soda yake inaladha inayopendwa zaidi sokoni wakaja na kampeni ya “ThePepsi challenge” iliyoenda sokoni kuiposition pepsi k**a soda yenye ladha bora zaidi kuliko Cocacola

The Pepsi challenge iliipa kampuni ya pespi ongezeko kubwa la wateja wakitokea Cocacola

Katika kujibu mapigo, Kampuni ya Cocacola ikaaamua kubadili ladha ya soda yake na kuleta ladha mpya waliyo itambulisha k**a “New Coke”

Walijua hawajui,
Hili lilikua kosa kubwa zaidi walilowahi kulifanya katika uendeshaji wa kampuni yao kwani baada tu ya New Coke kuingia sokoni

Walipokea simu nyingi za malalakiko kutoka kwa wateja wao kutokana na kubdilisha ladha ya kinywaji chao pendwa

Wateja wenye hasira kali walifikia kuandana kuishinikiza Cocacola kuirudisha sokoni ladha ya asili ya Cocacola “original coke” wanayoipenda

Kwa mara ya pili kampuni ya Pespi ilitumia mwanya huo kusisitiza kuhusu ladha yake ya asili na tamu kwa kulaunch kampeni ya matangazo inayoonesha watu wakinywa pesa huku wakisema “the taste is gonna move you” na “you can’t beat the original”

Matangazo hayo yaliiongezea pespi umaarufu na kujizolea wateja wengi waliokasirishwa na Cocacola kubadilisha ladha ya asili

Ndani ya miezi mitatu tu kamppuni ya Cocacola iliziona athari a uamuzi wao na kuamua kuirudisha sokoni Cocacola yenye ladha ya asili ili kuwaridhisha wateja wao.

Kuanzia hapo dunia ikatambua Cocacola ilikua ni zaidi ya kinywaji. Muunganiko wa kihisia uliopo baina ya wanywaji wa kinywaji hicho na ladha yake hauwezi kuutenganisha

Somo kubwa tunalolipata hapa ni kwamba usije ukabadilisha chochote katika bidhaa bila kuwashirikisha wateja watoe mapendekezo yao. Hakikisha unapata data za kutosha kabla ya kufanya mabadiliko ili kuendelea kuipa brand yako heshima na kuendelea kuwaridhisha wateja wako.Wateja wana nguvu.

Je wewe ni mpenzi wa kinywaji gani kati ya pepsi na Cocacola?

Upo kwenye ajira na unatamani uanze kujiingizia kipato cha ziada na hujui pakuanzia? ebook yangu mpya ya Side Hustle Blu...
08/05/2023

Upo kwenye ajira na unatamani uanze kujiingizia kipato cha ziada na hujui pakuanzia?

ebook yangu mpya ya Side Hustle Blue Print itakupa muongozo wa njia rahisi zaidi unayoweza kuanza nayo kuingiza kipato cha ziada.

Kwa Watu 10 wa Mwanzo wataipata kwa Tsh 3,000 tu.

Address

Salasala
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SMB Consulting posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Category