Tourism for Development Centre

Tourism for Development Centre This is a new NGO which aim to bridge the gape between Tourism and development for the benefit of the Tanzanian
(12)

HABARI NA HISTORIA YA WAMAKONDE NA TAMADUNI ZA KUJICHORA, KUJITOBOA, KUJIKATA VIDELO NA KUCHONGA MENO.Wamakonde ni moja ...
08/02/2018

HABARI NA HISTORIA YA WAMAKONDE NA TAMADUNI ZA KUJICHORA, KUJITOBOA, KUJIKATA VIDELO NA KUCHONGA MENO.

Wamakonde ni moja ya kabila la kibantu linalopatikana kusini mwa nchi ya Tanzania na kaskazini mwa nchi ya Msumbiji. Lugha yao ya asili ni kimakonde ambacho chenyewe kina mgawanyiko wake kulingana na mazingira. Yaani kuna kimakonde cha Bara yaani kile kimakonde kilichochanganyika na Kiswahili, yaani Kimalaba.

Na kuna kimakonde cha ndanindani wanakiita Kimawia, hiki ndio kile kimakonde chenyewe kabisa cha asili, yaani mtu anaweza kuongea na usielewe k**a wewe sio Mmakonde wa kundi hili. Ukiwa hapa Tanzania Wamakonde wanapaikana mkoa wa Mtwara, hasa hasa Mtwara Mjini. Lakini kutokana na mabadiliko ya maisha wamakonde ni moja ya watu wanaosambaa sana japo hawasambai maeneo ya mbali.

Kwa ufupi tu neno Wamakonde/konde›msitu/ linamaana ya Watu wa Msituni, na hili jina walilipata baada ya mapambano ya kivita yaliopata kutokea maeneo tajwa takribani miaka 500 iliopita. Na kabla ya watu hawa kuitwa jina hili moja la kikabila walikuwa wakiitwa majina ya koo kulinga na maeneo yao. Siku tukipata nafasi tutajadili asili ya majina ya koo za kiafrika hasahasa Wabantu.

kwa ujumla Wamakonde wana utamaduni wao ambao ni uchongaji na tamaduni zingine k**a uchezaji wa ngoma ya Sindimba, Vyakula k**a Chikandanga na Ming’oko, matambiko na ususi. Lakini kutokana na kabila la Wamakonde kuingiliana na makabila mengine, kumekuwa na tamaduni ambazo wamakonde wamakuwa nazo. Hivyo kwenye makala hii tutajadili mambo k**a Kujichora, Kujitoboa, Kujikata Videlo Na Kuchonga Meno.

ILIKUWAJE MPAKA WAMAKONDE WAKAANZA, KUJICHORA, KUJICHANJA,KUCHONGA MENO NA KUKATA VIDOLE?

Inasimuliwa kuwa, Mnamo karne ya 16-19 yaani 1500-1800 biashara utumwa ilishamili sana maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki. Kulingana na masimulizi na baadhi ya maandiko yanasema kuwa, huko kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji kulikuwa na njia ya misafara ya Utumwa aliokuwa ikisimamiwa na Wamakua na baadae Wayao(rejea historia ya Wamakua). Hivyo katika kutekeleza biashara hii kulikuwa na uhuitaji mkubwa sana wa watumwa kutoka sehemu hizi. Na moja ya Kabila ambalo lilikubwa na biashara hii ni Wamakonde.

Historia inasema hivi, Kabla ya biashara ya utumwa Wamakonde hawakuwa na utamaduni wa kujichora, kujitoboa, kujikata, wala kuchonga viungo vya miili yao, isipokuwa utamaduni wao ulikuwa ni uchongaji wa vinyago. Lakini kutokana na uwepo wa biashara ya utumwa ndipo Wamakonde walipoamua kutafuta njia ya kupambana na biashara hiyo. Inasimuliwa kuwa, sifa ya mtumwa ilikuwa ni kuwa na nguvu, kuwa na muonekanomzuri na asiwe na majelaa wala alama za aina zozote mwilini.

Sasa Wamakonde waliamua kukata baadhi ya vidole, kuchonga meno, kutoboa midomo kwa ajili ya kuweka ndonya ili wafanyabiashara watakapo kuja wasiwachukue. kwani mtumwa alitakiwa kukamilika viungo vyote vya mwili na bila kuwa na majeraa. Hivyo idadi kubwa ya watumwa wa Kimakonde walikuwa wakiachwa hapo hapo, kwani mtumwa aliyekuwa akisafirishwa kwenda Zanzibar alipaswa kuwa mtu mwenye viungo vilivyokamilika.

Na kila wakati Wafanyabiashara walipokuwa wanafika kwenye maeneo ya Kimakonde hawakuchukua watumwa. Kwani walidhani kuwa,watu hawa wana ugonjwa wenye kuwatoa mapele na alama mbalimbali mwilini. Ifahamike kuwa, sio k**a wafanya biashara hao hawakujua kuwa Waafrika wana utamaduni wa kujichora, ila kwa Wamakonde ilikuwa taofauti. Kwani walikuwa hawachongi k**a sehemu ya urembo, hivyo alama hazikuwa nzuri na wakati mwingine Vidonda vyenye kutisha.

Na mara baada ya kuonekana kuwa endapo ukijichora huchukuliwi Utumwa jambo hilo likaendelea na likawa k**a sehemu ya maisha. Na mtu ambaye hakufanya hivyo alionekana k**a mtumwa. Na kwa kuwa watu waliogopa kutengwa na kuchukuliwa utumwani kila familia ilibidi wafanye hivyo japo mambo yalikuwa magumu, kwa mfano suala la kuchonga meno lilikuwa ni la hatari sana namaumivu.

Historia inasema kuwa, mara baada ya biashara ya utumwa kuisha mnamo karne ya 19, Wamakonde wamejikuta wakiendeleza utamaduni wa kuchonga meno, kutoboa ndonya na kujichora michoro usoni kwa kisu cha jadi. Na mpaka kipindi cha ukoloni ambapo Tanganyika ilikuwa chini ya Ujerumani kuanzia miaka ya 1890 mpaka miaka ya 1919, bado Wamakonde waliendeleza tamaduni zao.

Na hata kipindi cha Waingereza yaani kuanzia miaka ya 1920-1960, bado mambo yalikuwa hivyo. Lakini kuna mabadiliko, Kwani mwanzo ilikuwa ni kuzuia utumwa, lakini kwa wakati ule ilikuwa sehemu ya Urembo. Na k**a ni kijana hukuwa na chochote mwilini wewe ulionekana wa ajabu na sio mjanja wa mji. Na hauendani na wakati. Hivyo hata kukawa na wasanii maarumu wa kufanya kazi hizo kwa ubunifu na kwa gharama.

Kwa sasa tamaduni hizi za kujichora, kuchonga meno,kukata vidole na kutoboa midomo, zinaonekana kufa na ukiuliza sababu ya kufa ni kwamba, tamaduni hizo si sehemu ya Wamakonde, kwani zilianzishwa kutokana na utumwa na sasa utumwa haupo.

*Habari na historia hii ni sehemu ndogo sana ya historia ya kabila la Wamakonde. Hivyo mawazo yako yanahitajika sana katika kujengwa historia hii.

Source
Na: Mayuni Josefu

tfdc tunawatakia woote furaha na amani katika siku hii ya Simba duniani. #  # #
10/08/2017

tfdc tunawatakia woote furaha na amani katika siku hii ya Simba duniani.
# # #

Clouded leopard - India
06/08/2017

Clouded leopard - India

*Prof Maghembe apokea Mabilionea wa Dunia Serengeti* SERENGETI, Mara:23.07.2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Juma...
25/07/2017

*Prof Maghembe apokea Mabilionea wa Dunia Serengeti*

SERENGETI, Mara:23.07.2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, jana aliwapokea Mabilionea 26 katika Mbuga ya Serengeti.

Mabilionea hao walifuatana na wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Wageni hao ambao wanatoka katika club ya mabilionea ya YPO (Young Presidents Organisation) wanatoka mabara yote duniani.

Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa vivutio vya utalii barani Afrika na duniani.

Katika ziara hiyo ya nchi nane (8) ambazo ni: Uingereza, Rwanda, Tanzania, Maldeves, Nepal, Bhutan, Rajastan na nchi moja nyingine, wageni hao wamemwaga sifa kem kem kwa vivutio vya Tanzania.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Prof. Maghembe aliwakaribisha nchini Tanzania na kuwaambia kuwa maajabu ya Dunia yamebebwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

"Hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivorous) na wale wanaokula nyama (carnivorous) k**a ilivyo katika mbuga hiyo ya Serengeti.

Aidha, Prof. Maghembe aliwaeleza wageni wake kuwa uhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia.

Aliwaomba wageni hao wawe Mabalozi wa kuitangaza Tanzania k**a eneo pekee la amani lenye vivutio vyenye ubora wa pekee duniani.

Alisema hatua hiyo italeta watalii wengi nakuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokuwa kwa wastsni wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

Ends

happy mothers day to you all #  # # #  # #
14/05/2017

happy mothers day to you all
# # #
# # #

Tajirika na Kilimo cha Nyoka ,.Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwauaKilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye fai...
01/05/2017

Tajirika na Kilimo cha Nyoka ,.Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua
Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake. Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000 *K**a unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka 1.zingatia hali ya joto na hewa . Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku, 2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata. 3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai. Faida 3 za ufugaji wa nyoka 1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa. 2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu k**a panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa. **Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.

asante jamiiforums

# # #

BINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA.Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo ...
27/04/2017

BINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA.

Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikiria Rekodi ya kula Chumvi nyingi Duniani kwa sasa.

Mzee Ambilikile Panja ambaye alishuhudia Vitaa kuu zote Mbili za Dunia kwa ukaribu, anakadiriwa kuwa na Umri wa wa zaidi ya miaka 127 leo.

Mkazi huyo wa Kitongoji cha Izyika ambaye kwa sasa haoni wala Kusikia vyema amemsimlia mwandishi wa makala hii kuwa wakati wa Vita ya Maji Maji dhidi Wakoloni alikuwa tayari anachunga mifugo ya Baba yake Marehem Mwanyaluke Panja.

Mzee Ambilikile Panja Kabila Mndali kutoka Tarafa ya Bundali Ileje anasema, Wakati wa Vita ya Maji Maji "Wazazi wetu walitwambia tukiona Wazungu tuiache mifugo tukimbie kurudi nyumbani" anasema Mzee Panja.

Mzee Panja ambaye kwa sasa hawezi kusimama wala kutembea anasema, Vita ya Kalenga (Mkwawa) haikuwahi kufika kwao Ileje, Isipokuwa Vita ya Pili ya Dunia ilifika mpaka Mbozi.

Anasema Vita ya Hi**er, (Vita ya Pili ya Dunia) ilianza Wakati yeye akiwa ameshakimbia kutoka Ileje na kuhamia Mbozi (Kijiji cha Ihanda) baada ya Kupora Mke wa Chifu. Anasema yeye mwenyewe alishuhudia Mzungu aliyekuwa na Nywele mwili Mzima mithili ya Mnya akiwa amekimbia kujiokoa na Maadui zake. "Tulipo muona huyo Mzungu, tulidhani ni Mnyama kumbe ni Binadamu", anasema kwa Kindali huku akishusha Kicheko hafifu kilichofuatiwa na Kikohozi cha Ukongwe.

Mzee Ambilikile anasema Wakati wa Vita ya Hi**er tulilazimika kuchimba Mashimo {Mahandaki} ya kujificha kuleee Lwibhaaa (Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ihanda)

Mzee Panja ambaye mtoto wake wa Kwanza Marehemu Leonard Panja alifariki dunia kutokana na Uzee, mwaka 2014 akiwa na Umri wa miaka 98 anasema Marafiki zake wote, pamoja na Maadui zake wakiwamo Machifu aliokuwa anapingana nao, wote wameshatangulia mbele za haki amebaki pekee yake.

"Mimi nilitoka Kapelekeshi nikaenda kuishi Ibungu Itumba na baadae nikahamia hapa Mbozi. Hapa nilikuja na Mke wangu Mkubwa Agnes Mlawa na Watoto wangu watatu Leonard, Lassary na Pitros pamoja na Zacharia Panja na marehemu Mbonasi Panja (watoto wa ndugu zake)"
anasimulia mzee Panja.

Mzee Ambilikile kwa sasa ni Kikongwe asiyeweza kufanya Chochote bila ya Msaada wa mtu mwingine. Mzee kwa sasa hubebwa au kusukumwa na Kiti cha Magurudumu (Wheel Chair) ambayo humsaidia kwa ajili ya kusogezwa eneo moja hadi jingine.

Kwa sasa Mzee huyu anaishi na Mke wake wa 4 Bi. Atusajigwe Mshani wa Mwisho katika wake zake ambaye naye kwa sasa ni mzee mwenye Umri wa miaka 89 licha ya Kuwa ana umri sawa na Mzaliwa wa tano wa Mzee Ambilikile Panja.

Aidha, kwa mujibu wa mtoto wa Mwisho wa Mzee Panja ambaye ndiye hutunza takwimu za familia ya Mzee Ambilikile, Ndugu Lawrence A. Panja; Baba yake anadhaniwa alizaliwa mwaka 1890 Katika Kijiji cha Kapelekeshi Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.

Kikongwe huyu hajulikani popote zaidi ya Vijiji vinavyo mzunguka. Hata Serikali ya Wilaya tu haijui kuwa ina Raia wake mwenye Umri mkubwa namna hii.

Ni wajibu wetu k**a Nchi kusaidia dunia kumfahamu Babu huyu mwenye Umri Mkubwa kuliko wengine. Ni jukumu la Wandishi na Vyombo mbalimbali pamoja na Mitandao ya Kijamii kuujulisha Ulimwengu Mtu huyu anayeishi maisha ya mwendo wa Marathon kwa sasa.

Sio kila siku tunafuatilia na kusimulia mambo ya Mataifa ya Nje wakati MUNGU na sisi katupendelea. K**a tumeweza kuuambia ulimwengu Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na sio Kenya basi na hili tunaweza tukiamua.

Mwisho naomba Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini Mashirika ndani na nje ya Nchi, pamoja na Wananchi mbalimbali kujitolea kumsaidia na kumtunza Mzee Panja ambaye kwa Umri wake ni k**a Lulu iliyosalia Duniani kwa sasa.
Shukran kwa Mwandishi wa Makala hii ni Ndugu Abel Sichembe

Email [email protected]
Share, Like, Coment, Re post, Sambaza mpaka iwafikie Guineas World of Record.
# # # #

Lion attack.Pole sana kwa muathirika wa tukio hili. Mungu akupiganie afya yako ndg yangu
25/04/2017

Lion attack.
Pole sana kwa muathirika wa tukio hili. Mungu akupiganie afya yako ndg yangu

Hamadi mtaani kwako unamkuta kwenye hali hiyo.Swali Je utamsaidia kumtoa au unapita mbaali sana? #  # #
20/04/2017

Hamadi mtaani kwako unamkuta kwenye hali hiyo.
Swali Je utamsaidia kumtoa au unapita mbaali sana?

# # #

MEDIA OFFICIAL FROM ISRAEL VISIT TANZANIATeam of journalists from Israel on the way to Gombe National Park in new effort...
19/04/2017

MEDIA OFFICIAL FROM ISRAEL VISIT TANZANIA
Team of journalists from Israel on the way to Gombe National Park in new efforts which is being conducted by Tanzania Tourist Board to pe*****te the Israel Market.

Timu ya wanahabari kutoka Israel ikielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kuandika habari zitakazolenga kuwahamasisha Waisrael kutembelea hifadhi za magharibi.
Source: Utalii hazina yetu

Bush soccer, tourist against maasai. #  # #
18/04/2017

Bush soccer, tourist against maasai.
# # #

Je hao ni aina tofauti za Faru?K**a ndio eleza yupi ni yupi? #  # #I LOVE TANZANIA
14/04/2017

Je hao ni aina tofauti za Faru?
K**a ndio eleza yupi ni yupi?

# # #
I LOVE TANZANIA

This is how it is #  #I LOVE AFRICA
13/04/2017

This is how it is
# #
I LOVE AFRICA

Hahahahaaaa mtoto ni mtoto bwana.  # # #   love Africa.
12/04/2017

Hahahahaaaa mtoto ni mtoto bwana.
# #
# love Africa.

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana.Nilalapo nakuota wewe, niamkapo n...
10/04/2017

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana.
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama weee.
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo woteee.

MJUE MTANZANIA anayeshikilia rekodi Afrika ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa muda mfupi.Gaudence Lekule (31) k...
30/03/2017

MJUE MTANZANIA anayeshikilia rekodi Afrika ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa muda mfupi.

Gaudence Lekule (31) kutoka Marangu anashikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa muda mfupi wa saa 8 na sekunde 36.

Rekodi ya kwanza iliwekwa na Simon Mtui aliyetumia saa 9 na sekunde 20 mwaka 2006.

Mpaka sasa rekodi ya dunia inashikiliwa na Karl Egloff kutoka Ecuador aliyetumia saa 6 na sekunde 53.

Kijana huyu anayeshiriki michezo ya kupanda milima kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo ,Dkt Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.

Meet Tanzanian mountain runner Mr Lekule who hold the record as first African to spend shortest time to climb and slump Mt Kilimanjaro.

Lekule (31), from Kiraracha, Marangu became the first African to spend 8 hours and 36 for a climb and return trip to from the mountain peak.

The first record of climbing Mount
Kilimanjaro was set by Simon Mtui by
spending 9:20 in 2006.

Lekule who holds the record of being the
first Mount Kilimanjaro climber who used
shortest time, called also for cooperation
from private institutions and the Government in sponsoring athletes for Mountain Run so that they become better internationally.

“I like to promote Tanzania worldly and I
have already received many invitations to go out to compete in the Mountain Run.

The World Record is held by Karl Egloff from Ecuador, who spent 6:53 to climb and slump Mount Kilimanjaro in 2014.

Thanks to Utalii_Tanzania

Wadau naomba majina ya hao ndege, kuna zawadi.
25/03/2017

Wadau naomba majina ya hao ndege, kuna zawadi.

hii nyingine tena, karibuni sana wadau.
09/09/2016

hii nyingine tena, karibuni sana wadau.

31/07/2016

Habari ya masiku wadau wetu wa utalii, Tfdc inapenda kuwataarifu kuwa kuanzia leo yeyote atakaye comment, share au kulike chochote kwenye page yetu atakiwa kaingia kwenye shindano la kushinda vifuatavyo:-
•Fedha taslimu
•Safari za kutembelea vivutio vya utalii.
•Vocha
•T shirts na zawadi zingine kibaaao.

Karibuni sana wadau. Washindi tutakuwa tunawachagua humu wenyewe.

Habari mbaya kwenye sekta yetu,  enyi wenye dhamana na hili tunawaomba mliangalie kwa jicho la tatu maana tunaelekea kuu...
01/07/2016

Habari mbaya kwenye sekta yetu, enyi wenye dhamana na hili tunawaomba mliangalie kwa jicho la tatu maana tunaelekea kuua utalii wetu.
# # #
# # # #

JE WAJUAKiboko anapokuwa amekasirika, jasho lake linageuka kuwa jekundu.Kinachotokea hapo anapokuwa amekasirika mapigo y...
30/06/2016

JE WAJUA
Kiboko anapokuwa amekasirika, jasho lake linageuka kuwa jekundu.

Kinachotokea hapo anapokuwa amekasirika mapigo ya moyo huenda kasi na kuzungusha damu kwa speed zaid ya kawaida(tacchycardia),kitendo hicho husababisha vinyweleo kupanuka na hivyo kiasi kidogo cha damu huchanganyikana na jasho na kutolewa nje hali ambayo hibadili rangi ya jasho lake kuonekana nyekundu!!!!

# # #

The second richest country in wildlife resources after Brazil Tanzania ni nchi ya pili kwa utajiri wa wanyama pori baada...
25/06/2016

The second richest country in wildlife resources after Brazil
Tanzania ni nchi ya pili kwa utajiri wa wanyama pori baada ya brazil.... Ndege wa Tanzania, naipenda Tanzania.

Hifadhi ya Kitulo awali ilijulikana k**a Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredrick Elton kupita eneo hili mnamo mwaka 187...
21/06/2016

Hifadhi ya Kitulo awali ilijulikana k**a Elton Plateau baada ya Mvumbuzi Fredrick Elton kupita eneo hili mnamo mwaka 1870. Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) ilichukua eneo hili kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.

Baadaye ikageuzwa kuwa shamba la ng'ombe ambalo lipo hadi leo. Kutokana na umuhimu wa eneo hili wadau mbalimbali wa mazingira walipendekeza eneo hili litangazwe kuwa hifadhi ya taifa ili kulinda umaridadi wa maua na mimea adimu inayopatikana ndani ya eneo hili.

Shamba la ng'ombe

Mwaka 2005, Kitulo ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, Msitu wa Livingstone na bonde la Numbi kiasi cha kilometa za mraba 412.9 ndani ya mwinuko wa mita 2100 na 3000.

Hifadhi hii inasifika kwa kuwa na maua aina mbalimbali na zaidi ya aina 30 hupatikana Kitulo pekee na maeneo kusini mwa Tanzania.

Maua ya Kitulo

Pia ndilo eneo pekee Tanzania ambapo ndege aina ya Tandawili machaka (Denhams Bustard) wana makazi. Wapo aina mbalimbali ya ndege k**a vile Mpasua mbegu mweusi (Kipengere seed eater) na wengineo.

Jamii mpya ya nyani (Lophocebus Kipunji) waligunduliwa mwaka 2003 Kitulo. Hifadhi hii ina uwanda wa tambarare, mabonde, vilima na maporomoko ya maji. Ndani ya msitu, kuna miti aina ya cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiriwa kuwa mirefu kuliko yote duniani.

Kitulo inafikika kwa gari kutoka Chimala, kilometa 78 Mashariki mwa mji wa Mbeya. Reli ya TAZARA hupita karibu na hifadhi ya kitulo. Pia unaweza kufika ukitokea Zambia kupitia Tunduma au Malawi kupitia Karonga kwa barabara.

Asante mdau wetu Anna Kihalu

Swaumu kaliiiii....Sisi Simba wa Serengeti tunawatakia swaumu njema. #  # #
11/06/2016

Swaumu kaliiiii....
Sisi Simba wa Serengeti tunawatakia swaumu njema.
# # #

Once upon a time, an elephant and a dog were pregnant at same time. Three months down the line the dog gave birth to six...
09/06/2016

Once upon a time, an elephant and a dog were pregnant at same time. Three months down the line the dog gave birth to six puppies. Six months later the dog was pregnant again, and nine months on it gave birth to another dozen puppies. The pattern continued.
On the eighteenth month the dog approached the elephant questioning, _"Are you sure that you are pregnant? We fell pregnant on the same date, I have given birth three times to a dozen puppies and they are now grown to become big dogs, yet you are still pregnant. Whats going on?"._
The elephant replied, _"There is something I want you to understand. What I am carrying is not a puppy but an elephant. I only give birth to one in two years. When my baby hits the ground, the earth feels it. When my baby crosses the road, human beings stop and watch in admiration, what I carry draws attention. So what I'm carrying is mighty and great."._

Thank you so much Naila Yusuph for this story.

Credits to

DONT SHOOT BY GUN SHOOT BY CAMERA!

Pictures of the day. Nawatakia usiku mwema. #  # #
06/06/2016

Pictures of the day.
Nawatakia usiku mwema.
# # #

Leo ni siku ya Mazingira duniani. Tfdc-tz inapenda kwakumbusha watanzania wote kwa ujumla kuwajibika ipasavyo kutunza ma...
05/06/2016

Leo ni siku ya Mazingira duniani.
Tfdc-tz inapenda kwakumbusha watanzania wote kwa ujumla kuwajibika ipasavyo kutunza mazingira yetu. Mazingira ndio uhai wetu na ndio uhai wa utalii wetu pia.
Tunza mazingira ili nayo yatutunze sisi na vizazi vyetu.
Asanteni.

03/06/2016

Je unafaham kwamba, kipindi cha kupandana Simba hutumia siku 7 kwa shuhuli hiyo bila kula wala kunywa??
Na dume humpanda jike kila baada ya dk 15.

Address

Mbezi Tank Bovu, Oilcom
Dar Es Salaam
P.O.BOX33471

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tourism for Development Centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tourism for Development Centre:

Videos

Share

Nearby travel agencies