18/04/2024
TUKUTANE HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI, MEI MOSI 2024.
Haya sasa, tunakutana tena ndani ya hifadhi ya taifa ya mikumi, mapema kabisa tarehe 1 ya mwezi huu wa 5 kwa mwaka huu wa 2024. Moja ya hifadhi tulivu na inayofikika kirahisi.
TAREHE YA SAFARI
Hii tutaifanya tarehe 1 ya mwezi wa 5 k**a nilivyoeleza hapo awali, ni siku muhimu ya sisi wapenda wanyama, wapenda mbugani, na wapenda uhifadhi bila kusahau wenye mahaba makubwa na wanyamapori kujumuika na kufurahi pamoja.
MUDA WA KUKAA HIFADHINI
Safari hii itakuwa ni ya siku mbili (2) ambapo utalala hifadhini siku moja (1) k**a ambavyo tangazo linajieleza.
BEI ELEKEZI KUHUSU SAFARI
Hapa kwa wewe mtanzania wa kawaida, utalipa shilingi za kitanzania elfu tisini (90,000/=) wakati kwa wageni ambao sio watanzania, watalipa kiasi cha dolla mia mbili ($ 200) tu.
MJUMUISHO WA BEI
Katika hiyo pesa utakayokuwa umelipia, basi kutakuwa na mjumuisho wa vitu mbali mbali k**a vile;-
1. Kiingilio cha hifadhini
2. Malazi kwenye hema
3. Chakula na vinywaji baridi (vinywaji laini) wakati wa safari
4. Usafiri wa gari utakayotumia mbugani na;-
5. Gharama za waongoza watalii wazoefu na waliobobea kwenye kazi hii.
MAWASILIANO
Unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia namba za simu ama kwa barua pepe zinazopatikana hapo kwenye tangazo juu.
NB: Uzuri wa safari ni kuwa unakutana na watu tofauti tofauti ambapo mnaweza kupeana fursa za maisha, pia kubadirisha ujuzi. Connection zinaanzia hapa k**a ulikuwa hufahamu hilo.
Hapa sijamaanisha connection k**a zile za kwa dada wa taifa mange kimambi la hashaaa! Ni connection za kupeana michongo ya mjini na jinsi ya kupata pesa ππ
Mtembea bure sio sawa na mkaa bure. Tukutane sasa hifadhi ya taifa ya mikumi chap kwa haraka bila kusitasita.