04/03/2024
NIWAKUMBUSHE TENA BAADHI YA WATU
MAANA NAONA HUU UCHAFU UMEZIDI SASA (HACKERS)
SOMA NA SHARE KWA WENGINE.
Kuna mchezo sasa hivi watu wanalalamika account kuwatag huku zikiwa na picha za matusii huku wakishindwa kujuwa kwa nini imekuwa hivyo
Hao ni hackers ambao wengi wapo Kenya huwa wanawaingia kwa kuwaambia wapo tayari kuwa unganisha wapate fund za UNCEF FOUNDATION huku wakiwaambia wawatumie namba zao na kukuambia ujaze taarifa fupi
Sasa ukijichanganya ukajaza wale jamaa wanafanya kitu kimoja ukiwapa namba yako wanaingia facebook
Wakiingia wanaenda sehemu ya kuforget PASSWORD ya FACEBOOK watakuambia kuna CODE unatumiwa hapo ili ku prove ombi lako la KUPOKEA FEDHA, sasa wee kwa kuwa unatamaa ya hela unawatumia CODE.
Kitendo cha kuwatumia CODE ndo kosa linaanzia hapo wakiingiza code kule tuu wabadili password then wanamiliki account yako wanwatafuta watu wako wa karibu na kuwaomba hela huku wakiendelea na mchezo wa kuwaibia watu wako account zao k**a kawaida kupitia wewe maana k**a mtu wako wa karibu akikutumia link na wewe silazima utamwamini hapo ndo kosa
Cha kuzingatia nenda kwenye SETTING ya simu yako kwenye swala la mtu aku TAG lazima u prove k**a hujaonekana public hii itakuwa msaada kwako
Pia zingatia hakuna hela ya bure bila kufanya kazi nje na hapo mtaibiwa hadi muuombe poo
Zingatia usipokee link ambayo haiko salama https hiyo s hapo mwisho inaonyesha link ni salama
Ikija http hiyo achana nayo kabisaa utaliswa vibaya sana
PIA KUNA KITU KINAITWA [CLICK BITE]
Hii ni ile umetumia PICHA CHAFU na kwakuwa watu wengi wanapenda kuziangalia kisiri siri huwa wanafungua lakini hawapati kile wanachokiona, maana yake ina ku REDIRECT na kukupeleka kwwnye MATANGAZO ambayo wewe ukifungua tu yeye kwenye BLOG yake au WEBSITE yake inapata watembeleaji wengi na hivyo yeye kulipwa kutokana na MATANGAZO.
USIFUNGUE LINK.
PLEASE SHARE KWA WENGINE WAJUE.