18/11/2024
Wakili wa Mahak**a Kuu ya Tanzania Fernidand Makole, amesema kwa mujibu wa sheria za Tanzania, taratibu za uk**ataji zinamtaka Polisi akienda kumk**ata Mtuhumiwa kwanza ajitambulishe na aonesha hati ya uk**ataji (arrest warrant) akiwa na gari la Polisi linalotambulika hivyo waliohusika kwenye tukio la Mfanyabiashara Deogratius Tarimo wawe ni Polisi au Watu wengine wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwakuwa wamekiuka sheria.
“Hii ya kuk**ata holela ndio inatengeneza makosa ya utekaji ambayo ni ya jinai, maoni yangu Mtu akija hajajitambulisha usikubali akuk**ate, akija Mtu na silaha kwa kutumia nguvu k**a Tarimo alichofanya hapa ni kujitetea mwenyewe (self defence), kwa mujibu wa sheria kuna utetezi binafsi, kwahiyo Mtu akija kukuk**ata na hajajitambulisha jitetee hata ukienda Mahak**ani ukiwa na kosa utasema nilikuwa najitetea kulinda usalama wangu binafsi” ameeleza Wakili Makole kwenye mahojiano na
Baada ya tukio hili la kutaka kutekwa kwa Mfanyabiashara Deogratius Tarimo, Mawakili/Wanasheria mbalimbali wa Tanzania wamejitokeza kuikumbusha jamii ya Watanzania sheria inasemaje pale wanapofuatwa kuk**atwa na Polisi ambapo Wakili Jebra Kambole ameandika yafuatayo.
Usikubali kuk**atwa na Mtu;
1. Kavaa kiraia
2. Gari halina No. au No za kiraia
3. Watu ambao hawajatoa vitambulisho
4. Watu wasiokwambia kosa lako na kwamba uko chini ya ulinzi.
5. Watu wasio na hati ya uk**ataji!!