Chuma 255

Chuma 255 Blog hii ni kwa ajili ya Habari,Music na Entertaiment. [email protected] +255 712 222244

Cool and respectfull life time, out going,down to earth love making friends,i love all hate me?

INNALILAH WAINA ILAH RAJIUN ALLAH AKUPE KAULI THABITI NDUGU YETU JUMANNE MWISONGO.Amefia 🇬🇧 na ndio alikuwa akiishi kwa ...
28/08/2024

INNALILAH WAINA ILAH RAJIUN ALLAH AKUPE KAULI THABITI NDUGU YETU JUMANNE MWISONGO.
Amefia 🇬🇧 na ndio alikuwa akiishi kwa muda baada ya kuondoka Morogoro Msiba upo UK.

26/08/2024
*MAKABIDHIANO YA OFISI MOROGORO*.Jumatano 21 Agosti, 2024.Morogoro.Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mheshimiwa *M***AKILAKALA*...
21/08/2024

*MAKABIDHIANO YA OFISI MOROGORO*.
Jumatano 21 Agosti, 2024.
Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mheshimiwa *M***A
KILAKALA* leo Jumatano 21 Agosti, 2021 amekabidhiwa Ofisi na alivekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa *REBECA
NSEMWA* aliyehamia Wilaya ya Bahi.
Wilaya hiyo ya Morogoro ina Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na ina Majimbo Matatu ya uchaguzi, Tarafa 7 na Kata 60 na Wakazi 859,145.

Makabidhiano na mazungumzo hayo yamefanyika mbele ya
Wajumbe wa K**ati ya Usalama Wilaya, Watumishi wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya Mheshimiwa
*PASCAL MWENDASHULE KIHANGA* Naibu Meya
Mheshimiwa *SELF ZAHORO CHOMOKA*, Katibu wa CCM
Wilaya ya Morogoro Vijijini ndugu *EMMANUEL MBAMANGE*, Madiwani, Wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata na Wakuu wa Taasisi mbalimbali zilizopo katika Manispaa ya Morogoro.
Baada ya makabidhiano na mazungumzo hayo Mheshimiwa
KILAKALA ataenda kuzungumza na Watumishi na Watendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

, Dkt. SamiaNiRaisWetu.
.

Mama Anakuja ??K**a Ukipata Nafsi Yakuongea Na MamaKuhusu Mapungufu Ya Morogoro UtamwambiaNini ?     # tanzania
01/08/2024

Mama Anakuja ??

K**a Ukipata Nafsi Yakuongea Na Mama
Kuhusu Mapungufu Ya Morogoro Utamwambia
Nini ?

# tanzania

Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi na kumteu...
01/08/2024

Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue,
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume
hiyo.
Rais amefanya uteuzi huo siku mbili baada ya juzi July 29,2024 kutangaza uamuzi wa Serikali kuunda k**ati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi Nchini wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).
Rais amewateua pia Wajumbe wa Tume hiyo akiwemo Prof.
Florens Luoga, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Prof. M***a Juma Assad ambaye alikuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wengine ni Leonard Mususa, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania, CPA.
Aboubakar Mohamed Aboubakar, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, Mshauri wa Masuala ya Sheria.

Wengine ni David Tarimo, Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kodi, PC,
Balozi Maimuna Kibenga Tarishi, Katibu Mkuu Mstaafu na Rished Bade, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Treni ya Umeme ya Kisasa (SGR) imeonekana kuwavutia wasafiri wengi tangu ilipoanzakutumika chini, ikisafirisha abiria za...
11/07/2024

Treni ya Umeme ya Kisasa (SGR) imeonekana kuwavutia wasafiri wengi tangu ilipoanza
kutumika chini, ikisafirisha abiria zaidi ya abiria 4,000 kwa siku, kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Idadi ya abiria wanaosafiri kwa treni hiyo kwa siku imefikia
kiwango hicho katika kipindi ambacho safari pekee zinazofanyika ni katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.
Kwa mujibu wa TRC, idadi ya abiria wanaosafiri kwa SGR kwa
siku inatarajiwa kuongezeka mara mbili ya wanaotumia sasa, pindi zitakapozinduliwa safari za Dodoma mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa kawaida ingechukua zaidi ya mabasi 70 kusafirisha abiria 4,000, jambo linaloonyesha dalili ya mapinduzi katika sekta ya usafirishaji hasa utakapoanza ule wa mizigo.

Mtoto amepotea leo saa  11 jioni tunaishi azimio pomba la abood mtoto anaitwa Brighton Kingililwe ana miaka 3 amepotea a...
05/07/2024

Mtoto amepotea leo saa 11 jioni tunaishi azimio pomba la abood mtoto anaitwa Brighton Kingililwe ana miaka 3 amepotea akiwa amevaa sweta jeusi ya kupauka lina picha ya spider mbele suruali ya kijivu (Track) na yebo za njano hizo alizo vaa hapo. Naomba nisaidie ndugu
‪+255 652 443 030‬

K**ati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeamua riba ya Benki Kuu(CBR) inayotozwa ...
04/07/2024

K**ati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeamua riba ya Benki Kuu
(CBR) inayotozwa kwa benki zinazokopa kutoka benki hiyo
kuendelea kuwa asilimia sita kwa robo mwaka itakayoishia
mwezi Septemba mwaka huu.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanyika kwa kikao cha
K**ati ya Sera ya Fedha na kutathmini hali ya uchumi na vihatarishi ambavyo vinaonesha kwa kipindi cha mwezi
Januari hadi Juni 2024 mfumuko wa bei umedhibitiwa na kuendelea kubaki chini ya lengo la asilimia tano.
Akitoa taarifa hiyo mkoani Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha kutoka Benki Kuu Dkt. Yamungu
Kayandabila amesema maamuzi ya k**ati yamezingatia mtazamo chanya wa uchumi wa dunia ambapo matarajio ni kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei duniani, kuimarika
kwa ukwasi katika masoko ya fedha duniani na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia.
Wakati huo huo Dkt. Yamungu ameweka bayana kuwa
upatikanaji wa fedha za kigeni umeanza kuimarika kutokana
na ongezeko la fedha za kigeni kutoka kwenye mauzo ya
tumbaku, dhahabu na shughuli za utalii, huku akiba ya fedha za kigeni ikiendelea kuwa ya kutosha kwa kuwa na zaidi ya Dola Billioni tano za Kimarekani, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa muda wa miezi minne.

DAR ES SALAAM - SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limeongeza safari za treni ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam n...
03/07/2024

DAR ES SALAAM - SHIRIKA la Reli Tanzania
(TRC) limeongeza safari za treni ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro ambapo kuanzia Julai 5, abiria wataanza kutumia treni ya haraka (express train) isiyosimama vituo vya kati.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Jamila
Mbarouk leo Julai Mosi imesema TRC itaendelea kuongeza
safari za kwenda na kutoka Dar es Salaam na Morogoro.
“Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00
asibuhi na 01:10 jioni na itaondoka Morogoro saa 12:20
asubuhi na saa 01:30 siku na treni ya kawaida itaondoka Dar es Salaam 03:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na kwa Morogoro itaondoka saa 03:50 asubuhi na 10:20 jioni.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani humo Irv...
03/07/2024

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo.
Mutegeki amek**atwa na nyara hizo za Serikali wilaya ya Kibondo Julai 2,2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara
ya meno ya tembo kutoka wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo
Burundi.
Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mauaji ya tembo katika misitu na hifadhi zilizopo katika wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Taarifa kutoka wilayani humo inaonyesha kuwa kuna jitihada za kuficha suala hilo kwa kutengenezwa mazingira ya rushwa ili kulimaliza jambo hilo ambalo ni uhujumu uchumi.

CHAGUO NI LAKO MWANA MOROGORO!!!RATIBA YAKO.... USAFIRI WAKO......
15/06/2024

CHAGUO NI LAKO MWANA MOROGORO!!!
RATIBA YAKO.... USAFIRI WAKO......

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SCSalim Abdallah Muhene (Try Again) ametangaza rasmi kung’atuka katika nafasi ya...
11/06/2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC
Salim Abdallah Muhene (Try Again) ametangaza rasmi kung’atuka katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC uamuzi ambao unaashiria MO Dewji
anarudi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.

“Sisi k**a Viongozi imefikia hatua sasa tuiokoe Simba SC,
mtu pekee ambaye naona anaweza kuitoa hapa Simba na kuipeleka mbele zaidi ni MO Dewji, sijui k**a ataridhia ila nimemuomba MO Dewji arudi kuwa Mwenyekiti wa Bodi”
Salim Abdallah
Try Again alianza kushika nafasi ya juu ya Vongozi ndani ya Simba SC 2017 k**a Kaimu Rais wa Simba SC, Mjumbe wa Bodi na hatimae Mwenyekiti wa Bodi.

Ubovu wa barabara inayotoka Lukobe Mwishokuelekea Mazimbu jirani na Barabara kuu ya Morogoro - Dodoma, umekuwa kero kwa ...
08/06/2024

Ubovu wa barabara inayotoka Lukobe Mwisho
kuelekea Mazimbu jirani na Barabara kuu ya Morogoro - Dodoma, umekuwa kero kwa wakazi wa kata Lukobe eneo la Lukobe juu Manisapaa ya Morogoro, hali ambayo imepelekea kupanda kwa gharama za maisha hasa upande wa usafiri na Maji na kuwalazimu Wananchi kufunga njia, ili kufikisha ujumbe kwa Serikali.
Wakizungumza Leo Wananchi hao wamesema hakuna barabara inayofika katika Kata yao, kwani iliyokuwepo awali imefungwa kupisha ujenzi wa njia ya Treni ya Mwendokasi na
kupelekea kubuni njia mbadala katika eneo la shule jambo ambalo limepelekea wao kukusanyika na kufungua njia hiyo
kwani inaleta usumbufu kwa Wanafunzi.
Wamesema, licha ya haribifu wa barabara lakini hakuna upatikanaji wa maji Safi na salama na kwamba wananunua dumu moja kwa shilingi 800.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi - CCM Wilaya ya Morogoro mjini, Fikiri Juma akiongozana na viongozi mbalimbali wa Serikali, ametembelea eneo hilo na kumuelekeza Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo, pamoja na kuwataka LATRA kurejesha huduma ya usafiri.
Naye Meneja wa TARURA Mohamed Mwanda, ambaye amesema amepokea maagizo hayo kutoka Kwa Mwenyekiti
na kuhaidi utekelezaji wa haraka, ili Wananchi wa eneo hilo wapate huduma ya Barabara kwa wakati.

Tanzia
08/06/2024

Tanzia

UMEWAHI KUWEKEWA HII ?
07/06/2024

UMEWAHI KUWEKEWA HII ?

Taarifa iliyotolewa na Benki kuu ya Taifa (BoT) inaeleza kuwani kosa kisheria kuitumia pesa kutengeneza mfano wa ua amba...
06/06/2024

Taarifa iliyotolewa na Benki kuu ya Taifa (BoT) inaeleza kuwa
ni kosa kisheria kuitumia pesa kutengeneza mfano wa ua ambalo mara nyingi hutumika k**a zawadi

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga Afrika, Miguel Gamondi amesema fainali ya kesho dhidi ya Azam FC, kwao hawaichukulii k**a m...
01/06/2024

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga Afrika, Miguel Gamondi amesema fainali ya kesho dhidi ya Azam FC, kwao hawaichukulii k**a mechi ya kisasi, bali fursa ya kurekebisha makosa waliyofanya kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya
NBC walipofungwa 2-1.
“Kwenye mpira hakuna kulipiza kisasi. Ukienda kwenye
mchezo kwa nia ya kulipa kisasi hutokuwa na mchezo mzuri.
Namheshimu mpinzani wangu Azam FC, lazima twende tukacheze mchezo wenye mbinu nzuri ili tuweze kuibuka na
ushindi,” amesema Miguel Gamondi ambaye kupitia kauli zake amethibitisha pia kwamba ni mwanafalsafa.

Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametangazwa Mshindi kwenyeuchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti ...
29/05/2024

Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametangazwa Mshindi kwenye
uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya
Nyasa ambapo amemuangusha aliyekuwa anatetea kiti hicho,
Mchungaji Peter Msigwa.

Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo May 29,2024 katika Mji wa Makambako Mkoani Njombe yametangazwa usiku huu
baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa kupiga kura.

Sugu ameshinda kwa asilimia 51 huku Mchungaji Msigwa
akipata asilimia 49 ya kura zilizopigwa.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mshindi ni
Frank Mwakajoka ambaye ni Mbunge wa zamani wa Tunduma.

liliyanscateringservice and 851 others mwananchi_official Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa safari...
25/05/2024

liliyanscateringservice and 851 others mwananchi_official Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa safari ya treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma inatarajiwa kuanza Julai 25 mwaka huu.
Mbarawa ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu SGR kipande cha Dar es Salaam na kujiridhisha kuwa treni hiyo itaanza na mandalizi
yanaendelea vizuri.
“Nimekagua miundombinu ya madaraja na vivuko pamoja na treni kazi inakwenda vizuri na Julai 25,2024 tunatarajia kuanza safari ya Dar es Salaam kwenda Dodoma,” amesema Mbarawa.
Pia Waziri Mbarawa amesema kuwa nauli ya treni hiyo itakuwa rafiki kwa kila Mtanzania ataweza kusafiri kuanzia
daraja la kwanza mpaka daraja la tatu.
Katika kuhakikisha safari ya treni hiyo inaanza bila kuwepo changamoto, Mbarawa amesema Juni treni hiyo itaanza safari ya Dar es Salaam mpaka Morogoro na mifumo ya tiketi itakuwa tayari na kutoa wito kwa Watanzania kuanza kusafiri kwa treni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kuwa vivuko vya magari na vya watembea kwa miguu, vitakamilika mapema mwezi ujao na
wataongeza vivuko vingine vya watembea kwa miguu

Address

Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chuma 255 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Chuma 255:

Videos

Share