05/04/2023
PUBLIC NOTICE
Imepita Muda kidogo nikiwa kimya kutokana na kubanwa na majukumu ya kikazi. Sambamba na jukumu kubwa la utengenezaji wa website mpya ya Halisia Afrika pamoja na urekebishaji mkubwa wa website ya We Cab Tours and Safaris nimefanikiwa kuhamisha ofisi yetu ya mkoa wa Kigoma kutoka sehemu ilipokuwa awali (Gezaulole Gungu - Kigoma) kwenda Barabara ya Che Guevara ambayo inatambuliwa na wengi k**a barabara ya Bagwe - Katonga katika mabanda ya Aqua Opposite na Tanesco Power Station.
Nina furaha kuwajulisha kuwa ofisi hii imekamilika na imeanza kutoa huduma. Na kuanzia week ijayo tutazindua website yetu ya Halisia Afrika ambayo mpaka muda huu imekamilika kwa 80% - 85%.
Haikuwa kazi rahisi na tunaelewa umuhimu kutengeneza website hii from scratch. Website hii imetumia muda, akili, na resouce fedha kuifikisha ilipofikia. Tunafanya kazi usiku na mchana ili malengo ya uzinduzi kwa week ijayo yatimie. Kongole kwa Necia Technology kwa juhudi kubwa mliyoifanya katika kazi hii. Haijawa na haitakuwa rahisi, ila imani huzaa imani.
Bado haijawa rasmi ila unaweza kutembelea www.halisiaafrica.com ili kuona maendeleo ya website hii na kwa nia njema unaweza toa maoni yako. Pia unaweza tembelea offical page ya Halisia Africa Travels and Tours na kutuunga mkono kwa ku like na ku follow. Tunatambua kazi ya website ni endelevu na kwamba hata baada ya uzinduzi matengenezo na maboresho yataendelea.
Ahsanteni sana wadau wangu na rafiki kwa kuniunga mkono. Mnanipa moyo sana wa kupambana.
Ahsanteni sana.
Juma Shabani Sendekwa
CEO We Cab Tours and Safaris and Halisia Afrika
Our goal is to liberate this generation to explore the globe. Through our individual experiences and group travel meet-ups, we annually assist hundreds or thousands of travelers in organizing stress-free vacations