05/12/2024
WAJUE WAASISI WA "CHICKENS IN THE BUS"
Mwanzoni mwa kitabu changu cha “Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences,” nimeelezea chimbuko la hiki kitabu. Nimemtaja rafiki yangu mSomali Bashe Said k**a chanzo muhimu:
"There was another source of inspiration. In 2007, Bashe Said, a Somali friend of mine, asked me to write a column for his newspaper, the "African News Journal." I wrote "Chickens in the Bus," "Do You Have an Accent?," "It Takes a Village to Raise a Child," "African Time," and "Will I Ever be a Millionaire."
Bashe mwenyewe ndio huyu anayeonekana nami katika hii picha ambayo tulipiga jana tarehe 11 Mei, 2024 hapa chuoni St. Olaf. Nimebahatika kuwa na wadau wengi k**a Bashe, wa mataifa mbali mbali, ambao wako bega kwa bega nami. Ni baraka kubwa nami ninamshukuru Mungu daima.