LIM Safaris Co. Ltd

LIM Safaris Co. Ltd Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from LIM Safaris Co. Ltd, Travel Agency, 0754548192, Moshi.
(8)

Management ya Lim Safari's & Co Ltd Moshi Kilimanjaro inapenda kutoa pole sana kwa tawi la Lim Safari's Morogoro kufuati...
23/07/2017

Management ya Lim Safari's & Co Ltd Moshi Kilimanjaro inapenda kutoa pole sana kwa tawi la Lim Safari's Morogoro kufuatia kifo cha mfanyakazi mwenzao Dada Leila kilichotokea usiku wa trh 22nd kuamkia 23rd July huko Morogoro.
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu Dada Leila mahali pema peponi. Ameen!

Oscar Peter
Maneger,
Lim Safari's & Co Ltd.

Safari ikiwa imesimama kupisha hali ya barabara kutengemaa kufuatia maji mengi kujaa juu ya barabara katika eneo katikat...
13/05/2017

Safari ikiwa imesimama kupisha hali ya barabara kutengemaa kufuatia maji mengi kujaa juu ya barabara katika eneo katikati ya Hotel ya Liverpool na Kituo cha mabasi Mombo. 11 May 2017.

TUKIWA TUNATIMIZA MIEZI (3) MITATU.tangu tulipoanza kuiunganisha milima na tamaduni za kanda ya kaskazini (ARUSHA NA MOS...
06/04/2016

TUKIWA TUNATIMIZA MIEZI (3) MITATU.
tangu tulipoanza kuiunganisha milima na tamaduni za kanda ya kaskazini (ARUSHA NA MOSHI) na milima na tamaduni ya kanda ya mashariki (MOROGORO) Hatukuwa na kazi nyepesi, japo tumekuwa na kazi ya kujivunia. Tumekutana na changamoto nyingi, kubwa ni abiria wengi kutokuwa na imani na makampuni mageni ya usafirishaji, changamoto hii haikutusumbua sana kwa kuwa tuliitambua kabla ya kuanza huduma zetu, lakini k**a kampuni yenye uzoefu tulikabiliana na kila changamoto tuliyokutana nayo na kubadilika muda mwingine kulingana na mahitaji ya soko au ili kuendana na tamaduni za abiria wetu tunaowahudumia, wahudumu wetu nao wamekumbana na changamoto kadhaa lakini wamezimudu na wanaendelea vizuri na majukumu yao.
Lim Safari's & co ltd inapenda kuwashukuru sana wote mlio na mnaoendelea kutuunga mkono, lakini pia tunakaribisha maoni, nasaha, ushauri na hata malalakiko juu ya mapungufu yetu katika huduma zetu, ili tuendelee kutoa huduma bora kabisa.
Karibuni sana...!

Tunawatakia kila la kheri katika kusheherekea sikukuu hii muhimu.Ahsanteni sana..!
27/03/2016

Tunawatakia kila la kheri katika kusheherekea sikukuu hii muhimu.
Ahsanteni sana..!

K**a kampuni tumependezwa, vutiwa, farijika sana kwa namna mnavyotuunga mkono.Mungu awabariki sana!
12/02/2016

K**a kampuni tumependezwa, vutiwa, farijika sana kwa namna mnavyotuunga mkono.
Mungu awabariki sana!

Wakati tumetimiza mwezi mmoja tangu tuanze route hii ya Arusha Moshi Morogoro hapo January 08, 2016.Ni nini maoni yako k...
12/02/2016

Wakati tumetimiza mwezi mmoja tangu tuanze route hii ya Arusha Moshi Morogoro hapo January 08, 2016.
Ni nini maoni yako k**a mdau wetu kuhusu huduma zetu?

Maoni yenu ni muhimu sana kabla hatujaanza route yetu nyingine mpya ya Dar - Mtwara.
Karibuni....!

Hatufanyi kazi kwa kushindana nani atawahi kuondoka ama kufika baina yetu na makumpuni pinzani, tunafanya kazi kwa kuong...
24/01/2016

Hatufanyi kazi kwa kushindana nani atawahi kuondoka ama kufika baina yetu na makumpuni pinzani, tunafanya kazi kwa kuongozwa na dira yetu ambayo ni, mapinduzi katika usafirishaji wa abiria, vifurushi na mizigo, usalama na utulivu kwa abiria wetu, na huduma za ndani na nje ya basi zinazokwenda na wakati. Kamwe hatufanyi kazi kwa mazoea, bali tunafanya kazi kutokana na matakwa ya wakati, kwa kuhakikisha abiria anaitumia nauli yake mpaka senti ya mwisho na anashuka katika ngazi ya mwisho ya mabasi yetu akiwa anatabasamu na asie na malalamiko.
Karibuni LIM Safari's.

LIM Safari's tunajivunia kuwaunganisha abiria wetu na kuwa familia moja...!

Tukiwa tunatoza nauli chini kidogo ya nauli elekezi za SUMATRA, tungali bado tunahakikisha abiria wetu anatumia kila sen...
24/01/2016

Tukiwa tunatoza nauli chini kidogo ya nauli elekezi za SUMATRA, tungali bado tunahakikisha abiria wetu anatumia kila senti katika nauli yake akiwa nasi safarini, tutakupa p**i, tutakupa soda au maji, tissue zipo wala usijifikirie kuomba, vitunzia taka vya kutosha tunavyo. Pia ukiishiwa na chaji tuna USB ports chini ya seats zetu, utatuita na tutakuunganishia, wahudumu wetu huongea kwa sauti za chini na k**a kuna matangazo, tutawatangazia kupitia vipaza sauti vilivyomo ndani, usawa wa juu ya viti vyenu.
UNAPOSAFIRI NA Lim Safari's TUNAKUHAKIKISHIA SAFARI YENYE UTULIVU na WAHUDUMU nadhifu na wenye UPENDO. KARIBUNI SANA!

1. Burudani ya TV2. Kipoza hewa3. Mfumo wa kuchajia smart phones kwa USB
14/01/2016

1. Burudani ya TV
2. Kipoza hewa
3. Mfumo wa kuchajia smart phones kwa USB

Hii ni kuonesha heshima na unyenyekevu wetu mkubwa kwenu ninyi watu wa Morogoro. Na vile mnavyotuunga mkono..!
14/01/2016

Hii ni kuonesha heshima na unyenyekevu wetu mkubwa kwenu ninyi watu wa Morogoro. Na vile mnavyotuunga mkono..!

Wakati ingizo letu jipya la Arusha Morogoro Higer T 735/736 DFX zikikabiliwa na na changamoto za kiufundi, T 735 DFX iki...
14/01/2016

Wakati ingizo letu jipya la Arusha Morogoro Higer T 735/736 DFX zikikabiliwa na na changamoto za kiufundi, T 735 DFX ikiwa na matatizo katika mfumo wa burudani, tv na mic, na T 736 DFX ikiwa na matatizo katika mfumo wake wa upoozaji vinywaji (fridge) zinaingia kwenye matengenezo huko Jijini Dar es Salaam, tunawaingizia toleo letu jipya kabisa kuanzia kesho trh 15 - 01 - 2016. Yutong T 217/221 DGC karibu sana!

Ahsanteni sana watu wa Morogoro kwa mapokezi na upendo mnaotufanyia, kwa namna mnavyotuunga mkono japo ni wageni wa njia...
10/01/2016

Ahsanteni sana watu wa Morogoro kwa mapokezi na upendo mnaotufanyia, kwa namna mnavyotuunga mkono japo ni wageni wa njia yenu, ila nasi tumewaonesha umahili wetu wa kutoa huduma za ubora na viwango vya juu, tunahakikisha kuwa hatupo katika majaribio, bali tumedhamiria kuwafanyia mapinduzi makubwa katika huduma za usafirishaji. Tunawapenda na KARIBUNI SANA!

09-01-2016Morogoro tumefika kwa mara ya pili. Katika  huduma zetu tunazotambia. Usafi ni moja wapo. KARIBUNI SANA
09/01/2016

09-01-2016
Morogoro tumefika kwa mara ya pili. Katika huduma zetu tunazotambia. Usafi ni moja wapo. KARIBUNI SANA

Tumepata mapokezi makubwa kutoka kwa wakazi wa Morogoro jana tulipotia mguu kwa mara ya kwanza kabisa, na tumepata uungw...
09/01/2016

Tumepata mapokezi makubwa kutoka kwa wakazi wa Morogoro jana tulipotia mguu kwa mara ya kwanza kabisa, na tumepata uungwaji mkono mkubwa asubuhi ya leo 09-01-2016, ukizingatia abiria wengi waliozoea kutembelea maeneo ya Kaskazini wanaifahamu LIM na wana imani kubwa na huduma za kampuni hii. KARIBUNI SANA!

Basi letu T 735 DFX likiwa hotelini katika safari yake ya kwanza kabisa kati ya Arusha na Morogoro trh 08 /01/2016Karibu...
08/01/2016

Basi letu T 735 DFX likiwa hotelini katika safari yake ya kwanza kabisa kati ya Arusha na Morogoro trh 08 /01/2016
Karibuni sana!

Tumeamua kuiunganisha Milima ya kaskazini na Milima ya Mashariki, Mila za Kaskazini na Mila za Mashariki kupitia Mabasi ...
08/01/2016

Tumeamua kuiunganisha Milima ya kaskazini na Milima ya Mashariki,
Mila za Kaskazini na Mila za Mashariki kupitia Mabasi yetu yenye huduma bora kabisa!

Kesho tarehe 08th January 2016 tunatia mguu kwa mara ya kwanza kabisa Mkoani Morogoro. Hatuendi huko kujifunza tunaenda ...
07/01/2016

Kesho tarehe 08th January 2016 tunatia mguu kwa mara ya kwanza kabisa Mkoani Morogoro. Hatuendi huko kujifunza tunaenda kuwaonyesha uzoefu wetu katika usafirishaji wa abiria, mizigo na vifurushi. Karibu ujionee huduma zetu, kwetu abiria ni rafiki wa kweli.

Kwa Morogoro muone
Hamisi Kindamba 0718 238008

Kwa Arusha muone
Dada Aisha 0752 033980

Kwa Mosho muone
Saidy 0754 548192

Sara fupi ya wanafamilia, uongozi, wafanyakazi na wadau (wateja wa kudumu) wa LIM Safari's wakiliombea ingizo jipya la m...
04/01/2016

Sara fupi ya wanafamilia, uongozi, wafanyakazi na wadau (wateja wa kudumu) wa LIM Safari's wakiliombea ingizo jipya la mabasi yetu, katika hafla fupi iliyofanyika jana 03rd Jan 2016 tayari kwa (route) safari zetu mpya ambazo tutazitangaza baadae.
Karibuni sana!

02/01/2016

Tuna uzoefu mkubwa katika usafirishaji abiria, huduma zetu ni bora, usafi kwa mabasi yetu ni mila yetu.
Ndio maana tunakaribia kutambulisha njia (route) mpya hivi karibu.
TUNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA...!

01/01/2016

Address

0754548192
Moshi
P.O.BOX1747

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LIM Safaris Co. Ltd posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category